5 – Kuelekea Qiblah
Mswaliji anapaswa kuelekea isipokuwa katika swalah ya Sunnah akiwa juu ya kipando kwa msafiri. Katika hali hiyo ataswali kuelekea upande wowote ambao kipando chake kinaelekea. Yule mwenye kushindwa kuelekea Qiblah kwa sababu ya khofu au sababu nyingine, ataswali kwa namna yoyote atakayoweza. Ama wasiokuwa hao wawili, basi swalah yao haisihi isipokuwa kwa kuelekea Ka´bah. Ikiwa yuko karibu na Ka´bah, basi ni lazima kwake kuelekea Ka´bah kwa kuilenga yenyewe. Akiwa mbali, basi aelekee upande wake.
Ikiwa Qiblah haijulikani akiwa mjini, basi atauliza na atatumia dalili kwa Mihraab za waislamu. Akikosea, basi atalazimika kurudia swalah. Ikiwa Qiblah haijulikani akiwa safarini, basi atafanya ijitihada na kuswali na hatolazimika kurudia.
Ikiwa watu wawili wenye kujitahidi watatofautiana, basi mmoja wao hamfuati mwenzake. Kipofu na mtu wa kawaida watamfuata yule wanayemwamini zaidi miongoni mwao.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 23
- Imechapishwa: 10/10/2026
5 – Kuelekea Qiblah
Mswaliji anapaswa kuelekea isipokuwa katika swalah ya Sunnah akiwa juu ya kipando kwa msafiri. Katika hali hiyo ataswali kuelekea upande wowote ambao kipando chake kinaelekea. Yule mwenye kushindwa kuelekea Qiblah kwa sababu ya khofu au sababu nyingine, ataswali kwa namna yoyote atakayoweza. Ama wasiokuwa hao wawili, basi swalah yao haisihi isipokuwa kwa kuelekea Ka´bah. Ikiwa yuko karibu na Ka´bah, basi ni lazima kwake kuelekea Ka´bah kwa kuilenga yenyewe. Akiwa mbali, basi aelekee upande wake.
Ikiwa Qiblah haijulikani akiwa mjini, basi atauliza na atatumia dalili kwa Mihraab za waislamu. Akikosea, basi atalazimika kurudia swalah. Ikiwa Qiblah haijulikani akiwa safarini, basi atafanya ijitihada na kuswali na hatolazimika kurudia.
Ikiwa watu wawili wenye kujitahidi watatofautiana, basi mmoja wao hamfuati mwenzake. Kipofu na mtu wa kawaida watamfuata yule wanayemwamini zaidi miongoni mwao.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 23
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/17-sharti-ya-swalah-kuelekea-qiblah/