16. Msimamo wa Salaf walioafikiana juu ya sifa za Allaah

Hapa ni baadhi ya maneno ya maimamu juu ya maudhui haya:

1 – Imepokelewa kutoka kwa al-Hasan al-Baswriy amesema:

”Mutwarrif alizungumza maneno yasiyokuwa na kifani kuhusu suala hili. Wakasema: ”Umesema nini, ee Abu Sa´iyd?” Akasema: ”Himdi zote njema ni stahiki ya Ambaye katika kumuamini ni kujahili yale ambayo hakujisifu Mwenyewe.”

81 – al-Awzaa´iy amesema:

”az-Zuhriy na Mak-huul walikuwa wakisema: ”Zipitisheni Hadiyth hizi kama zilivyokuja pasi na kuzifanyia namna.”

Wawili hao ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Maswahabah. Upokezi huo ni Swahiyh.

82 – Imesihi kwamba al-Waliyd bin Muslim amesema:

”Nilimuuliza Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy, al-Layth bin Sa´d na al-Awzaa´iy kuhusu Hadiyth kuhusu sifa. Wakasema: ”Zipitisheni kama zilivyokuja.”

Maalik alikuwa ni imamu wa Madiynah, ath-Thawriy alikuwa ni imamu wa Kuufah, al-Awzaa´iy alikuwa ni imamu wa Dameski na al-Layth alikuwa ni imamu wa Misri. Hawa ni miongoni mwa wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah wakubwa.

83 – Muhammad bin al-Hasan – ambaye ni mwanachuoni wa ´Iraaq – amesimulia maafikiano juu ya suala hilo. al-Laalakaa´iiy amepokea kwa cheni ya wapokezi wake akasema:

”Wanazuoni Mashariki mpaka Magharibi wameafikiana juu ya kuamini Qur-aan na Sunnah zilizopokea wapokezi wenye kuaminika kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba zinatakiwa kuaminiwa kuhusu sifa za Mola (´Azza wa Jall) pasi na tafsiri, maelezo wala kufananisha. Yule mwenye kufasiri kitu katika hizo basi ametoka nje ya njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akatengana na mkusanyiko. Hawakueleza wala kufasiri. Waliamini yale yaliyomo ndani ya Qur-aan na Sunnah na wakanyamaza. Yule mwenye kusema kama alivosema Jahm basi ametengana na mkusanyiko. Kwa sababu amemweleza kwa kisichokuwa kitu.

84 – Sufyaan bin ´Uyaynah amesema:

”Kila ambacho Allaah (Ta´ala) amejisifu Mwenyewe ndani ya Qur-aan basi kule kukisoma ndio tafsiri yake pasi na kufananisha wala kuyawekea namna.”

ash-Shaafi´iy amesema kuhusu huyu Sufyaan bin ´Uyaynah:

”Kama isingelikuwa yeye na Maalik, basi ingelipotea elimu ya Hijaaz.

85 – Aflah bin Muhammad amesema:

“Nilisema kumwambia Ibn-ul-Mubaarak: “Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Mimi nachukia kuzungumzia sifa za Mola.” Akasema: “Mimi ni mtu ambaye nachukia zaidi, lakini pindi Qur-aan inatamka kitu basi nasi tunakisema na pindi mapokezi yanapofikisha kitu basi tunakipokea.”

Baadhi ya maimamu wamesema:

”Ibn-ul-Mubaarak ni Kiongozi wa waumini katika kila kitu. Waislamu wameafikiana juu ya kuongoka kwake.”

  • Mhusika: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 82-84
  • Imechapishwa: 04/06/2024