Mola ni yule mwenye kuabudiwa na walimwengu na viumbe wote kama majini, watu, mbingu na ardhi. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mola na Muumbaji wavyo. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni wenu Ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kucha. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah wanaolingana Naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.” (02:21-22)

Amewaumba wote waliokuwa kabla yetu na wengine wote baada yetu, vyote kabla ya Aadam na baada yake. Amewaumba wote ili waweze kumuabudu na kumcha Yeye. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“… mpate kucha.”

Kisha (Subhaanah) akabainisha baadhi ya matendo Yake na kusema:

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً

“Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa.”

Ameifanya ardhi kuwa kama tandiko na paa yao ambapo wanaishi, wanajenga, wanalala na wanatembea. Ardhi imefanywa kuwa imara kwa milima. Ameifanya mbingu kuwa kama paa na sakafu yenye kufunika. Pamoja na hivyo watu ni wenye kuzipa mgongo alama Zake. Ameipamba kwa nyota, jua na mwezi:

وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً

“… akateremsha kutoka mbinguni maji.”

Ni maana kutoka kwenye mawingu:

فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ

“… akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu.”

Kuna aina mbalimbali za riziki sehemu kote. Allaah anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kisha Allaah (Ta´ala) akasema:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Basi msimfanyie Allaah wanaolingana Naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”

Bi maana wenza na washirika mkawa mnawaabudu pamoja Naye. Haijalishi kitu ni mamoja akawa ni sanamu, jini, Malaika au kitu kingine. ´Ibaadah ni haki ya Allaah peke yake. Hana mwenza, anayelingana Naye wala mfano Wake. Yeye ndiye Mungu wa haki. Washirikina walikuwa wakiabudu masanamu, majini, Malaika na vyengine pamoja Naye na wakiwaomba uokozi. Ndipo Allaah akawakataza na akawabainishia kuwa viumbe hivi havina haki ya kuabudiwa na haviwezi lolote isipokuwa kwa idhini na maamuzi ya Allaah (Subhaanah).

Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema katika Tafsiyr yake ya Qur-aan kwamba muumbaji wa vitu hivi mbingu, ardhi, matunda, mvua na vyenginevyo ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa na kutiiwa kwa kuwa Yeye ndiye Mola na Muumbaji wa vyote. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ

“Muabudiwa wenu wa haki ni Allah Pekee, hapana muabudiwa wa haki isipokuwa YeyeMwingi wa Rahmah, Mwenye kurehemu.” (02:163)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 07/12/2016