64 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Haamid bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Harawiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin Wahb ametuhadithia: Ibraahiym bin Sa´iyd al-Jawhariy ametuhadithia: Abu Ahmad az-Zubayriy ametuhadithia: Qays bin ar-Rabiy´ ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa Hudhayfah bin al-Yamaan, ambaye kutokana na ninavojua, amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ole wake ambaye hajui. Ole wake ambaye amejua na asifanyie kazi mara tatu.”[1]
65 – Ahmad bin ´Aliy bin Yazdaad al-Qaari’ ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ibraahiym bin ´Abdil-Malik al-Aswbahaaniy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Aliy bin Makhlad al-Farqadiy ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin ´Amr al-Bajaliy ametuhadithia: Faraj bin Fadhwaalah ametuhaidthia, kutoka kwa Sulaymaan bin ar-Rabiy´, mtumwa aliyeachwa huru na al-´Abbaas, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), aliyesema:
”Ole wake ambaye hajui. Allaah angelitaka angelimfunza. Ole wake ambaye hajui na hatendei kazi mara saba.”[2]
66 – Ibn Yazdaad ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ibraahiym ametukhabarisha: Muhammad bin ´Aliy al-Farqadiy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Amr ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Zakariyyaa ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, kutoka kwa Maymuun bin Mihraan, kutoka kwa Abud-Dardaa’ mfano wa hiyo[3].
67 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametukhabarisha: Husayn bin Abiy Ma´shar ametuhadithia: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, kutoka kwa Maymuun bin Mihraan, aliyesimulia kuwa Abud-Dardaa’ amesema:
”Ole wake ambay hajui. Ole wake ambaye anajua na asifanyie kazi mara saba.”[4]
68 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Ahmad bin Ishaaq bin Minjaab at-Twiybiy ametukhabarisha: al-Qaadhwiy Abul-Faraj Muhammad bin Ahmad bin al-Hasan ash-Shaafi´iy ametukhabarisha: Ahmad bin Yuusuf bin Khallaad ametukhabarisha: Muhammad bin Yuunus al-Qurashiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Daawuud al-Khuraybiy ametuhadithia: Ja´far bin Burqaan ametuhadithia, kutoka kwa Maymuun bin Mihraan, aliyesimulia kuwa Abud-Dardaa’ amesema:
”Ole wake ambaye hajui mara moja.”
Ibn Khallaad amesema:
”Ole wake ambaye hajui mara moja. Ole wake ambaye anajua na hatendei kazi mara saba.”
[1] Dhaifu kwa sababu ya Quraysh bin ar-Rabiy. Haafidhw Ibn Hajar amesema:
”Alikuwa mkweli, lakini alibadilika wakati alipokuwa mtumzima. Aidha mtoto wake aliongeza masimulizi yasiyokuwa katika maneno yake na baadaye yakasimuliwa.”
[2] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya al-Bajaliy na mwalimu wake Faraj bin Fadhwaalah wote wawili ni wanyonge. Isitoshe sikupata wasifu wowote wa Sulaymaan bin ar-Rabiy´, ambaye ni mtumwa aliyeachwa huru na ´Abbaas.
[3] Dhaifu kwa sababu ya Ismaa´iyl bin Amr, ambaye ni al-Bajaliy aliye kabla yake.
[4] Dhaifu kwa sababu ya Husayn bin Muhammad bin Abiy Ma´shar. adh-Dhahabiy amesema:
”Kwake kuna ulaini. Ibn-ul-Munaadiy amesema kuwa ”hakuwa mwenye kuaminika” na Ibn Qaaniy´ amesema ”ni mnyonge”.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 46-48
- Imechapishwa: 12/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)