Sehemu kubwa ya Hadiyth zilizopo kwa al-Bukhaariy na Muslim kuna uhakika ya kwamba yamesemwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Mosi ni kwamba kiasi kikubwa kilichotajwa kinakuwa sampuli hiyo na pili ni kwamba wanazuoni wamezipokea kwa ridhaa na kuzisadikisha. Jengine ni kwamba ummah mzima hauwezi kukubaliana juu ya kosa. Iwapo Hadiyth fulani ingekuwa ya uwongo na bado ummah mzima wanaisadikisha na kuikubali Hadiyth hiyo, basi hilo lingemaanisha wameafikiana juu ya kosa, jambo ambalo haliwezekani. Japokuwa bila ya maafikiano tunaweza kufikiria kuwa masimulizi fulani ni ya makosa au ya uwongo, ni kama vile, kabla ya utambuzi wetu wa maafikiano, tunaweza kuzingatia vivyo hivyo kwamba elimu, inayothibiti kwa nje au kupitia kipimo cha kudhania, ya kwamba haki ni kwa ndani tofauti na vile tulivyokuwa tunaitakidi. Kwa hiyo wanazuoni wakiafikiana juu ya hukumu, basi tunathibitisha kuwa hukumu hiyo imethibiti kwa ndani na kwa nje. Kwa sababu hiyo jopo kubwa la wanazuoni kutoka katika madhehebu yote wameafikiana ya kwamba Hadiyth, ambayo imesimuliwa na mpokezi mmoja na ambayo umah wameipokea kwa kuikubali, kuisadikisha na kuifanyia kazi, basi inapelekea elimu. Hili ndilo lililotajwa na waandishi wa vitabu vya misingi ya Fiqh katika wafuasi wa Abu Haniyfah, wa Maalik, wa Shaafi’iy na wa Ahmad bin Hanbal, isipokuwa tu kikundi kidogo cha wanazuoni wa zama za baadaye waliofuata maoni ya baadhi ya wanafalsafa ambao walipinga hilo. Hata hivyo wanafalsafa wengi, au wengi wao, wameafikiana na wanazuoni, Ahl-ul-Hadiyth na Salaf katika suala hilo. Hayo ni maoni ya wanazuoni wengi wa Ashaa´irah, kama vile Abu Ishaaq na Ibn Fawrak. Ibn-ul-Baaqillaaniy ndiye aliyekataa hayo na aka ، fuatwa na Abul-Ma’aaliy, Abu Haamiyd, Ibn ´Aqiyl, Ibn-ul-Jawziy, Ibn-ul-Khatwiyb, al-´Aamidiy na wengineo. Maoni ya kwanza ndio yaliyotajwa na Shaykh Abu Haamid, Abut-Twayyib, Abu Ishaaq na mfano wa hao katika maimamu wa ash-Shaafi´iy, al-Qaadhwiy ´Abdul-Wahhaab na watu mfano wao katika maimamu wa Maalikiyyah, Shams-ud-Diyn as-Sarkhasiy na watu mfano wao katika maimamu wa Hanafiyyah na Abu Ya´laa, Abul-Khattwaab, Abul-Hasan bin az-Zaaghuuniy na watu mfano wao katika maimamu wa Hanaabilah. Ikiwa maafikiano ya kusadikisha khabari fulani yanapelekea yakini, basi tegemezi katika jambo hilo ni maafikiano ya wanazuoni katika Hadiyth. Kama jinsi maafikiano tegemezi juu ya hukumu za Kishari´ah ni wale wanazuoni katika amri, makatazo na ruhusa.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 59-62
- Imechapishwa: 02/04/2025

Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 59-62
Imechapishwa: 02/04/2025
https://firqatunnajia.com/16-maafikiano-ya-ummah-juu-ya-al-bukhaariy-na-muslim/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket