Funga ina mambo yanayoiharibu ambayo inatakikana kwa muislamu aweze kuyajua ili ajiepushe nayo na atahadhari nayo kwa sababu yanamfunguza mfungaji na kumuharibia funga yake. Vifunguzi hivyo miongoni mwazo ni vifuatavyo:

1- Jimaa. Pindipo tu mfungaji atajamii basi funga yake imeharibika na atalazimika kuilipa siku hiyo ambayo amejamii ndani yake. Aidha – mbali na kulipa siku hiyo – atalazimika vilevile kutoa kafara. Kafara yenyewe ni kuacha mtumwa huru, asipopata au asipate thamani yake basi ni lazima kwake kufunga miezi miwili mfululizo, asipoweza kufunga miezi miwili mfululizo kutokana na udhuru unaokunalika katika dini, basi analazimika kulisha masikini sitini. Kila masikini atampa nusu ya Swaa´ ya chakula kinacholiwa kwa wingi katika mji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/382)
  • Imechapishwa: 24/04/2021