16. Hadiyth ”Anapotawadha mmoja wenu… ”

al-Haakim (1/181) amesema: Abu Ja´far Muhammad bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Baghdaadiy ametuhadithia: al-Miqdaam bin Daawuud ametuhadithia, kutoka kwa Taliyd ar-Ra´iyniy: ´Abdul-Ghaffaar bin Daawuud al-Haraaniy ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Abiy Bakr na Thaabit, ambaye ametuhadithia, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anapotawadha mmoja wenu na amevaa soksi za ngozi, basi aswali akiwa nazo na apanguse juu yake. Akitaka asizivue isipokuwa wakati wa janaba.”

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa sharti za Muslim. ´Abdul-Ghaffaar bin Daawuud ni mwenye kuaminika, hata hivyo si miongoni mwa wasimulizi wa Baswrah wenye kusimulia kutoka kwa Hammaad.”

al-Bayhaqiy (1/279) pia ameipokea  na akataja kwamba kwamba ´Abdul-Ghaffaar amefanyiwa ufuatiliaji na Asad bin Muusa, ambaye pia anaitwa simba wa Sunnah. Hadiyth ni yenye kupingana na zilizo Swahiyh. Haafidhw al-Bayhaqiy amesema:

”Kwa mujibu wa Ibn Swaa´iy, hajui mtu mwingine yeyote aliyeleta Hadiyth hiyo isipokuwa Asad bin Muusa.” Lakini imefanyiwa ufuatiliaji na Hadiyth yenye kuungana na ´Abdul-Ghaffaar bin Daawuud al-Haraaniy.  Hata hivyo si katika wasimulizi wa Baswrah wanaosimulia kutoka kwa Hammaad na hatambuliki – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.”

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 03/06/2025