Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

6- Tambua ya kwamba watu kamwe hawakuzusha Bid´ah isipokuwa waliacha Sunnah kiasi chake. Tahadhari Muhdathaat, kwani hakika kila Muhdathah ni Bid´ah, kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu na watu wake ni Motoni.

MAELEZO

Imekuja katika Hadiyth:

“Kila Bid´ah ni Motoni.”

“Utafarikiana Ummah huu katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moa.”

Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa Ahl-ul-Bid´ah watakuwa Motoni. Lakini hata hivyo wanatafautiana. Kuna wataokuwa Motoni kwa sababu ya kufuru yao, wengine watakuwa Motoni kwa sababu ya madhambi yao, kuna ambao watadumishwa Motoni milele na wengine ambao hukumu yao itakuwa ni kama wale walio na madhambi makubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 37
  • Imechapishwa: 03/12/2017