156. Yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake uko kila mahali

66 – Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Hanbal (164-241) – Allaah amrehemu, asalimishe roho yake na amjaalie Pepo iwe makazi yake!

226 – Yanayosimuliwa kutoka kwa imamu huyu katika mlango huu ni mazuri, yenye baraka na yaliyojaa kheri. Yeye ni mbebaji wa bendera ya Sunnah, mwenye subira katika mitihani na anayeshuhudiwa kuwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. Imepokelewa kutoka kwake kwa mapokeiz mengi kuwakufurisha wale wanaosema kuwa Qur-aan ni kiumbe, kuthibitisha Kuonekana kwa Allaah, ujuu na makadirio, kumtanguliza mbele Abu Bakr na ´Umar, kuona kwamba imani inaongezeka na kupungua pamoja na mengineyo katika mambo ya misingi ya dini ambayo maelezo yake ni marefu.

Yuusuf bin Muusa al-Qattwaan, mwalimu wake Abu Bakr al-Khallaal, ambaye:

“Kulisemwa kuambiwa Abu ´Abdillaah: ”Allaah (Ta´ala) yuko juu ya mbingu ya saba juu ya ´Arshi Yake, ametengana na viumbe Vyake na uwezo Wake na ujuzi Wake viko kila mahali?” Akajibu: “Ndio, Yuko juu ya ´Arshi Yake na hakuna mahali ambapo ujuzi Wake haupo.”[1]

[1] Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/568). al-Qattwaan alikuwa mwenye kuaminika na mmoja katika waalimu wake al-Bukhaariy. Alifariki mnamo 253. al-Khallaal aliyasikia hayo kutoka kwake. Cheni yake ya wapoezi ni Swahiyh.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 176
  • Imechapishwa: 19/01/2026
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy