Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

5- Yule asiyehukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah.

MAELEZO

Amesema (Ta´ala):

أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ

“Wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut.”[1]

Mwenye kuhukumu kinyume na Shari´ah hali ya kuwa ni mwenye kuhalalisha hilo anakuwa Twaaghuut. Ambaye anasema kuwa inafaa kuhukumiana kwa sheria za binadamu, kwa wajumbe kabla ya kuja Uislamu au wajumbe wa makabila na wa vijiji na kuiacha Shari´ah na akaona kuwa kufanya hivo inafaa, yanalingana na yale aliyoteremsha Allaah, akiona kuwa kufanya hivo ndio bora, yanalingana na Shari´ah, kwamba kufanya hivo ni halali peke yake ijapokuwa hatosema kuwa kunalingana wala kwamba ndio bora, bali akasema kuwa inafaa, huyu anazingatiwa kuwa ni Twaaghuut. Jambo hilo ni kwa andiko la Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ

“Wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut.”

Ameitwa kuwa Twaaghuut kwa sababu amevuka mpaka wake.

Ama yule mwenye kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah na wakati huohuo anakubali kwamba Shari´ah ndio lazima kuifuata, ambayo ni haki na kwamba yaliyo kinyume nayo ni batili na akajiona kuwa yuko katika batili, mtu huyu anazingatiwa kuwa amekufuru kufuru ndogo isiyomtoa mtu nje ya dini. Pamoja na hivyo yuko katika khatari kubwa na vilevile yuko katika njia inayoweza kumpelekea katika kufuru inayomtoa nje ya dini pale atapochukulia wepesi jambo hili.

Mwingine ni mtu anayetaka haki na anataka kuafikiana na hukumu ya Allaah (´Azza wa Jall) lakini hata hivyo asiwafikishwe. Anazingatiwa ni mwenye kupewa udhuru na mwenye kulipwa ujira. Lakini haijuzu kumfuata katika kosa. Katika hali hii kunaingia vilevile zile Ijtihaad za wanachuoni ambazo wamekosea ndani yake au Ijtihaad za makadhi katika mahakama pindi wanapojitahidi, wakafanya waliwezalo na wakajaribu kuifikia haki lakini hata hivyo wasiwafikishwe. Makosa yao ni yenye kusamehewa.

Kuhusu mwenye kuhukumu kinyume na Shari´ah pasi na kukusudia, bali ni kwa Ijtihaad  na akawa na upeo wa kufanya hivo katika wanachuoni na akajitajidi lakini hata hivyo asiisibu hukumu ya Allaah na akakosea katika Ijtihaad yake, huyu ni mwenye kusamehewa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Anapohukumu hakimu ambapo akajitahidi  kisha akapatia, basi ana ujira mara mbili. Na akijitahidi kisha akakosea, basi ana ujira mara moja.”

Kwa sababu hakukusudia kosa bali ameikusudia haki na amekusudia kuafikiana na hukumu ya Allaah. Pamoja na haya yote hakuwafikishwa. Mtu huyu anazingatiwa ni mwenye kupewa udhuru na kulipwa thawabu. Lakini haijuzu kumfuata katika kosa. Katika hali hii kunaingia vilevile zile Ijtihaad za wanachuoni ambazo wamekosea ndani yake au Ijtihaad za makadhi katika mahakama pindi wanapojitahidi, wakafanya waliwezalo na wakajaribu kuifikia haki lakini hata hivyo wasiwafikishwe. Makosa yao ni yenye kusamehewa.

[1] 04:60

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 304-306
  • Imechapishwa: 24/02/2021