Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
128 – Hatuoni kufaa kuwafanyia uasi viongozi na watawala wetu hata wakidhulumu.
MAELEZO
Hili ni suala kubwa na ni msingi miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hawaoni kufaa kuwafanyia uasi watawala wa waislamu:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yule mwenye kunitii mimi amemtii Allaah na yule mwenye kuniasi mimi amemuasi Allaah. Yule mwenye kumtii kiongozi amenitii mimi na yule mwenye kumuasi kiongozi ameniasi mimi.”[2]
Haijuzu kufanya uasi dhidi yao hata kama watakuwa watenda madhambi. Kwa sababu kiapo chao kinafanya kazi na utawala wao umethibiti. Jengine ni kwamba kufanya uasi dhidi yao kunapelekea katika madhara makubwa kama vile kuasi, mpasuko, kukosekana amani na makafiri kuwatawala waislamu. Shaykh-ul-Islaam amesema maneno yenye maana ya kwamba hakuna watu waliojivua katika utiifu wa kiongozi wao, isipokuwa hali yao baada ya kufanya uasi ilikuwa ni mbaya zaidi kuliko hali yao kabla ya kufanya uasi. Hali inakuwa hivyo hata kati ya makafiri. Wakiwafanyia uasi watawala wao basi kunakosekana amani na kunamwagika damu. Hawapati utulivu kamwe, jambo ambalo linaweza kushuhudiwa katika uasi uliotokea kwenye historia. Tusemeje juu ya kufanya uasi dhidi ya kiongozi wa waislamu? Kwa hivyo haijuzu kufanya uasi dhidi ya viongozi muda wa kuwa bado ni waislamu, hata kama watakuwa ni watenda madhambi. ´Ubaadah bin as-Swaamitw (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Tulikula kiapo cha usikivu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) juu ya kusikiza na kutii, katika uchangamfu wetu na yale tunayoyachukia, katika kipindi chepesi na kigumu, pindi mtu anapopendelewa juu yetu na kwamba tusivutane na watawala mpaka pale mtakapoona ukafiri wa wazi ambao tuna dalili kwao kutoka kwa Allaah.”[3]
Madhambi ya mtawala hayahalalishi kumfanyia uasi. Hilo ni tofauti na wanavyoona Khawaarij na Mu´tazilah. Wanaruhusu kufanya uasi dhidi watawala watenda maasi na wanaona uasi wao eti ni kuamrisha mema na kukemea maovu.
[1] 4:59
[2] al-Bukhaariy (7137) na Muslim (1835).
[3] al-Bukhaariy (7055-7056) na Muslim (1709).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 168-170
- Imechapishwa: 27/11/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 168-170
Imechapishwa: 27/11/2024
https://firqatunnajia.com/156-hatuoni-kufaa-kufanya-uasi-dhidi-ya-viongozi-wetu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)