Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
127 – Hatuoni kufaa kumsimamishia upanga yeyote katika ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa yule ambaye umemuwajibikia upanga.
MAELEZO
Haijuzu kumuua muislamu na kuihalalisha damu yake. Allaah ameiheshimisha nafsi yake kwa Uislamu. ´Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nimeamrishwa kuwapiga watu vita mpaka washuhudie ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Wakiyasema basi imesalimika kwangu damu na mali yao, isipokuwa kwa haki yake – na hesabu yao iko kwa Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Yeyote anayeonyesha Uislamu, akatamka shahaadah na asidhihirishe chochote katika yale mambo yanayochengua Uislamu, basi damu imeheshimishwa na wala haijuzu kumshambulia na kumwaga damu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika damu yenu, mali yenu na heshima yenu juu yenu ni haramu kama ilivyo siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu.”[2]
Je, kuna jambo khatari kushinda hili? Muislamu ana heshima kubwa zaidi mbele ya Allaah kushinda heshima ya Ka´bah. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda juu ya mimbari na akaita kwa sauti ya juu: ”Ee wewe ambaye umesilimu kwa ulimi wako na imani haijaingia ndani ya moyo wako! Usiwaudhi waislamu, usifuatilie aibu zao! Yule anayefuatilia aibu za ndugu yake muislamu basi Allaah atafuatilia aibu zake. Na yule ambaye Allaah atamfuatilia aibu zake basi atamfedhehesha hata kama atakuwa ndani kabisa ya nyumba yake.”
Siku moja Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliitazama Ka´bah na akasema:
”Ni namna gani ulivyo na utukufu! Lakini utukufu wa muislamu ni mkubwa zaidi kuliko utukufu wako.”[3]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema tena:
”Damu ya muislamu haihalaliki isipokuwa kwa moja ya mambo matatu: mtumzima anayezini, nafsi kwa nafsi nyingine au mwenye kuacha dini yake, anayefarikisha mkusanyiko.”[4]
1 – Mtumzima anayezini anakusudiwa ambaye ameoa na akamwingilia mke wake katika ndoa ambayo ni sahihi. Aidha ni lazima wazinzi hao wawili wawe wenye akili, wamekwishabaleghe na waungwana. Anayezini basi anatakiwa kupigwa mawe mpaka kufa.
2 – Muislamu anapomshambulia muislamu mwenzake na akamuua kwa dhuluma na uadui ambapo familia ya muuliwaji wakataka kisasi, katika hali hiyo atauliwa:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى
“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa [kulipiza] kisasi juu ya waliouawa.”[5]
Bi maana mmefaradhishiwa. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ
”Na humo Tumewaandikia ya kwamba uhai kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino na majaraha [kulipizana] kisasi.”[6]
3 – Mwenye kuritadi anatakiwa kuuliwa kwa sababu ya kuritadi kwake.
Mbali na hawa watu aina tatu damu ya muislamu ni yenye kuheshimiwa heshima kubwa.
Vivyo hivyo hukumu hiyo inawagusa waislamu madhalimu ambao wanawashambulia waislamu wengine. Wanatakiwa kupigwa vita kwa sababu wanataka kufarikisha umoja wa waislamu na kumfanyia uasi kwa kiongozi wao. Kwa ajili hiyo ni lazima kuwapiga vita:
وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ
“Ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana, basi suluhisheni baina yao. Lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah.”[7]
Damu yao ni halali kwa ajili ya kuzuia dhuluma zao, kuchunga umoja wa waislamu na kuhifadhi amani. Vivyo hivyo hukumu hiyo inawagusa majambazi:
إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Hakika si vyenginevyo malipo ya wale wanaompiga vita Allaah na Mtume Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha au watolewe katika nchi. Hayo ndio malipo yao duniani na Aakhirah watapata adhabu kuu; isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwatia mbaroni. Basi tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[8]
Watu hawa Allaah (´Azza wa Jall) amehalalisha kuwapiga vita kwa ajili ya kuzuia shari na mashambulizi yao.
[1] al-Bukhaariy (6924), Muslim (124) na Ahmad (67).
[2] al-Bukhaariy (67), Muslim (1679).
[3] at-Tirmidhiy (2032). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2032).
[4] al-Bukhaariy (6878), Muslim (1676).
[5] 2:178
[6] 5:45
[7] 49:9
[8] 5:33-34
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 166-168
- Imechapishwa: 27/11/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 166-168
Imechapishwa: 27/11/2024
https://firqatunnajia.com/155-makatazo-ya-kuwafanyia-vurugu-waislamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)