155. Hivi ndivo inavyoishilia ´Aqiydah yao

63 – Haafidhw Abu Ma´mar al-Qatw´iy (a.f.k. 236)

223 – Ibn Abiy Haatim amesimulia kutoka katika kitabu chake kutoka kwa Yahyaa bin Zakariyyaa bin ´Iysaa, kutoka kwa Abu Shu´ayb Swaalih al-Harawiy[1], kutoka kwa Abu Ma´mar Ismaa´iyl bin Ibraahiym, ambaye amesema:

“Maoni ya mwisho ya Jahmiyyah ni kwamba hakuna mungu juu ya mbingu.”

Abu Ma´mar ni mmoja wa waalimu zake al-Bukhaariy na Muslim. al-Bukhaariy pia amesimulia kutoka kwa mtu mwingine aliyepokea kutoka kwake. Alifariki mwaka wa 236 na alikuwa miongoni mwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah. Alikuwa na ujasiri kiasi cha kusema:

“Kama nyumbu wangu angeweza kuzungumza, angesema kuwa anafuata Sunnah.”

64 – Yahyaa bin Ma´iyn (a.f.k. 233), bingwa wa wenye kuhifadhi

224 – an-Najjaad amesema: Ja´far bin Abiy ´Uthmaan at-Twayaalisiy[2] ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Ma´iyn, ambaye amesema:

“Kama Jahmiy akikukuuliza ”Anashukaje?” basi muulize: ”Alipandaje?'”

Hayo maswali wote mawili yameondolewa inapokuja kwa Allaah (Ta´ala). Hakuna nafasi ya akili kuingilia kati katika jambo hili.

Yahyaa hajahitaji utambulisho. Yeye ndiye mnyumbulishaji wa bendera ya Hadiyth. Alifariki katika mji wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwaka wa 233.

65 – ´Aliy bin al-Madiyniy (a.f.k. 234), kiongozi wa Muhaddithuun

225 – Muhammad bin Ibraahiym amesimulia kutoka kwa Naafiy´: al-Hasan bin Muhammad bin al-Haarith ametuhadithia:

´Aliy bin al-Madiyniy aliulizwa nami nikiwa ninasikia kuhusu ´Aqiydah ya watu wa Mkusanyiko. Akajibu: “Wanaamini Kuonekana, Maneno, kwamba Allaah (´Azza wa Jall) Yuko juu ya mbingu na amelingana juu ya ´Arshi Yake.” Akaulizwa kuhusu Aayah isemayo:

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye yupamoja nao popote watakapokuwa, kisha siku ya Qiyaamah atawajulisha yale waliyoyatenda; hakika Allaah juu ya kila jambo ni mjuzi.”[3]

Akajibu: ”Soma sentesi ya kabla yake:

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِا

“Je, huoni kwamba Allaah anajua yale yote yaliyomo mbinguni na yale yote yaliyomo ardhini.” [4]

al-Bukhaariy amepokea kwa wingi katika ”as-Swahiyh” yake. Amesema juu yake:

“Sijawahi kujiona mdogo isipokuwa mbele ya Ibn al-Madiyniy.”

Alifariki katika mwezi wa Dhul-Qa’dah mwaka wa 234.

[1] Miongoni mwa watu wa kizazi chake ni Abu Shu´ayb Swaalih bin Ziyaad al-Muqriy ar-Raqqiy na Abu Shu´ayb Swaalih bin Mubashshir as-Swayrafiy. Wote wawili walikuwa wakweli. Abu Haatim ar-Raaziy ameandika kutoka kwao wote wawili, kama ilivyo katika kitabu cha mwanawe “al-Jarh wat-Ta´diyl” (2/1/404 na 416). Wasimulizi waliosalia ni madhubuti.

[2] Simjui huyu Ja´far. Hata hivyo an-Najjaad Abu Bakr Ahmad bin Salmaan al-Faqiyh alikuwa mwenye kuaminika na mwenye kuhifadhi. Alifariki mnamo 348.

[3] 58:7

[4] 58:07 Simjui al-Hasan bin Muhammad, Muhammad bin al-Haarith wala Naafi´. Mtunzi amenukuu kutoka katika cheni ya wapokezi ya Shaykh-ul-Islaam al-Harawiy.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 174-175
  • Imechapishwa: 19/01/2026
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy