Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

126 – Hatushuhudii juu yao ukafiri, shirki wala unafiki muda wa kuwa haijatudhihirikia chochote katika mambo hayo. Tunaziacha siri zao kwa Allaah (Ta´ala).

MAELEZO

Muislamu msingi wake ni uadilifu. Hii ni kanuni tukufu ambapo hatutakiwi kuwajengea dhana mbaya, kuwapeleleza wala kuwafuatiliafuatilia. Lakini tukidhihirikiwa na kitu, basi tutamuhukumu kwacho. Tusipodhihirikiwa na kitu, basi hatutakiwi kuwajengea dhana mbaya waislamu. Tunatakiwa kutangamana nao kutokana na yale yanayotudhihirikia kwao. Hatujawajibishiwa kuwapekua na kuwahukumu. Allaah hajatuwajibishia mambo hayo. Tunawadhania vyema na siri zao tunamtegemezea Allaah (Ta´ala). Hatujawajibishiwa kuwapeleleza watu na kuhusu hali zao. Ni lazima kumsitiri muislamu, kumdhania vyema na kujenga udugu kati ya waislamu:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ

“Hakika si vyenginevyo waumini ni ndugu, hivyo basi suluhisheni baina ya ndugu zenu.”[1]

[1] 49:10

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 165-166
  • Imechapishwa: 26/11/2024