Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
125 – Hatumkatii yeyote katika wao Pepo wala Moto.
MAELEZO
Hatumshuhudilii yeyote, pasi na kujali atakavyokuwa mwema na mchaji Allaah, kuwa ataingia Peponi. Kwani sisi hatujui mambo yaliyofichikana. Wala hatumshuhudilii yeyote, pasi na kujali atakuwa ni mtenda maasi kiasi gani, kwamba ataingia Motoni. Hatujui atakufa akiwa na hali gani. Haya yanahusu mtu mmoja mmoja kwa dhati yake. Sisi tunaangalia udhahiri peke yake. Wala hatumuhukumu mtu yeyote kuingia Motoni. Isipokuwa wale walioshuhudiliwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuingia ima Peponi au Motoni. Mfano watu hao ni wale Maswahabah kumi waliobashiriwa kuingia Peponi ambao ni wale makhaliyfah wanne waongofu, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Sa´iyd bin Zayd bin ´Amr bin Nufayl, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, az-Zubayr bin al-´Awaam, Abu ´Ubaydah ´Aamir bin al-Jarraah na Twalhah bin ´Ubaydillaah – Allaah awawie radhi wote!
Mtu mwingine aliyetolewa ushuhuda na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa kuingia Peponi ni Thaabit bin Qays bin Shimaas al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh).
Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ametoa mfano wa mtu wa tatu pale aliposema:
“Wakati tulipokuwa tumekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: “Atajitokeza kwenu mtu katika watu wa Peponi.” Akatokeza bwana mmoja katika watu wa Answaar. Ndevu zake zilikuwa zinadondoka maji kutokamana na wudhuu´ wake. Ameshika viatu vyake katika mkono wake wa kushoto. Siku ya pili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema maneno hayohayo. Akatokeza mtu yuleyule kama ilivyokuwa mara ya kwanza. Siku ya tatu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema maneno yaleyale. Akatokeza mtu yuleyule kama ilivyokuwa mara ya kwanza. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposimama, ´Abdullaah bin ´Amr al-´Aasw akamfuata na kusema: “Mimi nimegombana na baba yangu na nimeapa kuwa sintoingia nyumbani kwake kwa muda wa siku tatu. Hebu ungeniacha nikae kwako kipindi hicho, fanya hivo.” Akasema: “Sawa.” ´Abdullaah akaeleza kuwa alilala kwake kipindi cha nyusiku hizo tatu. Hakuona kuwa anaamka usiku kuswali chochote. Alichoona ni kwamba anapoamka, akajigeuza upande wa kitanda chake basi humtaja Allaah (´Azza wa Jall) mpaka anapoamka kwa ajili ya Fajr. ´Abdullaah amesema: “Licha ya kwamba sikumsikia anasema isipokuwa kheri tupu. Kulipopita siku tatu na nikakaribia kuyadharau matendo yake, nikasema: “Ee mja wa Allaah! Hakika hakukuwa kati yangu mimi na baba yangu ghadhabu wala kususana. Lakini mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema juu yako mara tatu: “Atajitokeza kwenu mtu katika watu wa Peponi.” Ukatokeza wewe mara tatu. Ndipo nikataka kukaa kwako ili nione ni yepi matendo yako na baadaye nikuigilize. Hata hivyo sikuona ukifanya matendo mengi. Ni yepi unayofanya mpaka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aseme namna ile juu yako?” Akasema: “Hakuna zaidi ya uliyoyaona. Wakati nilipoondoka akaniita na kusema: “Hakuna zaidi ya uliyoyaona, isipokuwa simfanyii nafsini mwangu yeyote katika waislamu ghushi wala simuhusudu kwa neema aliyopewa na Allaah.” ´Abdullaah akasema: “Hayo ndio yamekufikisha ulipo, na ndio ambayo hatuyawezi.”[1]
Kwa kumalizia ni kwamba pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapomthibishia mtu Pepo basi tunatakiwa kufanya vivyo hivyo. Ama kuhusu wengine tunawatarajia kheri. Kadhalika kuhusu kafiri mmoja mmoja kwa dhati yake hatusemi kuwa ataingia Motoni, kwa sababu anaweza kutubia na akafa juu ya tawbah na akayamaliza maisha yake katika hali nzuri. Hata hivyo tunachelea juu yake. Hapa ni pale ambapo inahusu mtu mmoja mmoja kwa dhati yake. Inapokuja kwa njia ya ujumla tunakata kabisa kwamba waislamu wako Peponi na tunakata kwamba makafiri ni katika watu wa Motoni.
[1] Ahmad (3/166).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 163-165
- Imechapishwa: 26/11/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 163-165
Imechapishwa: 26/11/2024
https://firqatunnajia.com/153-hatumthibitishii-yeyote-kuingia-peponi-wala-motoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)