153. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kwanza wa al-Anfaal

al-´Ayyaashiy amesema:

”Abu Baswiyr amesimulia kwamba amemsikia Abu ´Abdillaah akisema: “Yeyote atakayesoma Suurah at-Tawbah na al-Anfaal kila mwezi, basi hatopatwa na unafiki kabisa. Aidha atakuwa miongoni mwa wafuasi wa kweli wa kiongozi wa waumini na siku ya Qiyaamah kwenye meza za Peponi pamoja na wafuasi wake hadi watu wote wamalize hesabu yao.”[1]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokana na uongo huu wa kijinga. Kila muumini anaamini kuwa mambo ya ghaibu kama haya na ahadi za uhakika wa Pepo hutoka kwa Allaah tu na ni Mitume wake watukufu pekee wanaofikisha ujumbe wa aina hii. Wahy ulisitishwa baada ya kufariki kwa Mtume wa mwisho Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya na mengine yote yanayohusishwa na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh), Abu Ja’far, Abu ´Abdillaah na watu wengine wa Nyumbani yanatokana na uongo wa wazi wa ambao Allaah pamoja na waumini wanawatakasa kutokana nayo.

Tazama uwongo huu! Unafiki haupatikani katika pote lolote lile kama ulivyo miongoni mwa Shiy´ah Raafidhwah. Wao wanaamini uwongo (التقية) na kuuzingatia kwamba ni sehemu tisa kati ya sehemu kumi za dini yao. Hakika ni kifuniko kikubwa cha unafiki wao.

Hakika Ahl-us-Sunnah wana haki zaidi juu ya kiongozi wa waumini na watu wa nyumbani kwake kuliko Raafidhwah, ambao wanadai kuwa wao ni wafuasi wa watu wa Nyumbani na wafuasi wa watu wa Nyumbani, lakini wao kikweli ni maadui wa watu wa Nyumbani. Ni mamoja wanataka au hawataki. Ni mara ngapi wamewadhulumu watu wa Nyumbani na wamewachafua kwa uongo na uzushi ambao wanatengwa nao mbali!

Angalia uogo na wale wanaounga mkono pale wanapodai kwamba wafuasi wao hawatohesabiwa! Hata hivyo watu wote, ikiwa ni pamoja na Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi sallam), watahesabiwa ilihali mabwana hawa wao eti watakula kutoka kwenye meza za Peponi hadi watapomaliza hesabu zao!? Tunajiuliza nini kilichowafanya watu hawa hadi kufikia  ngazi hii? Je, ni shirki, upotevu, uongo, uzushi na mengineyo yasiyokuwa na kifani au kuna sababu nyingine?

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/46).

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 214
  • Imechapishwa: 18/02/2025