57 – Haafidhw Nu´aym bin Hammaad al-Khuzaa´iy (146-228)
216 – Muhammad bin Makhlad al-´Attwaar amesema: ar-Ramaadiy ametuhadithia:
”Nilimuuliza Nu´aym bin Hammaad kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ
“Yeye Ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi. Anajua yale yanayoingia ardhini na yale yatokayo humo na yale yanayoteremka kutoka mbinguni na yale yanayopanda humo – Naye yupamoja nanyi popote mlipo.”[1]
Akasema: “Maana yake ni kwamba hakuna kinachofichika Kwake kwa ujuzi Wake. Je, huoni pale Aliposema:
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ
“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao.”[2]
217 – Muhammad bin Ismaa´iyl at-Tirmidhiy amehadithia ya kwamba amemsikia Nu´aym bin Hammaad akisema:
“Yule mwenye kumfananisha Allaah na viumbe Vyake amekufuru. Yule mwenye kupinga yalwe aliyojisifu nayo Mwenyewe amekufuru. Hakuna katika yale aliyojisifu Mwenyewe nayo wala Mtume Wake ufananishaji.”[3]
Nu’aym bin Hammaad alikuwa na elimu iliobobea. Alikamatwa kuhusiana na fitina ya kuumbwa kwa Qur-aan, akatiwa jela na akafungwa minyororo mwaka wa 2295[4]. Allaah amrehemu! Aliishi miaka 80. al-Bukhaariy amehadithia kutoka kwake[5].
58 – Bishr al-Haafiy (151-227), mpaji nyongo wa kipindi hicho
218 – Alikuwa na ´Aqiydah iliyosimuliwa na Ibn Battwah katika kitabu chake “al-Ibaanah” na wengineo. Miongoni mwa yaliyomo ndani yake:
“Kuumini ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake, kama Atakavyo, kwamba Anajua kila mahali na kwamba Anasema na Anauumba. Basi kauli Yake ”Kuwa!” siyo kiumbe.”
´Abbaas bin Dahqaan ameeleza:
”Nilimwambia Bishr bin al-Haarith: “Napenda kuwa peke yangu nawe.” Akasema: “Kama unapenda hivo.” Siku moja mapema nikamuona anaingia ndani ya hema na akaswali Rak´ah nne kwa namna nisiyoweza. Nikamsikia akisema katika sijda yake: “Ee Allaah! Hakika Wewe unajua juu ya ´Arshi Yako ya kwamba unyenyekevu unanipendeza zaidi kuliko utukufu. Ee Allaah! Hakika Wewe unajua juu ya ´Arshi Yako ya kwamba umasikini unanipendeza zaidi kuliko utajiri. Ee Allaah! Wewe unajua juu ya ´Arshi Yako ya kwamba sipendelei kitu kingine juu ya mapenzi Yako.” Nilipomsikia nikaanza kulia kwa sauti na kuhema. Aliponisikia akasema: “Wewe unajua kuwa lau ningelijua ya kwamba uko hapa basi nisingeyasema hayo.”[6]
Bishr bin al-Haarith alifariki (Rahimahu Allaah) mwaka wa 229[7].
[1] 57:4
[2] 58:7 Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Ahmad bin Mansuur bin Sayyaar al-Baghdaadiy ar-Ramaadiy alikuwa mwenye kuaminika na mwenye kuhifadhi. Muhammad bin Makhlad al-´Attwaar alikuwa mwenye kuaminika na mkweli. Wasifu wake uko katika “Taariykh Baghdaad” (3/310-311).
[3] Mtunzi wa kitabu amepokea masimulizi haya kwa cheni ya wapokezi wake na akasema: Abul-Fidaa’ bin al-Farraa’ ametukhabarisha: Ibn Qudaamah ametuzindua: Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy ametuzindua: Ibn Khayruun na Abul-Hasan bin Ayyuub ametuzindua: Abu ´Aliy Shaadhaan ametuzindua: Ibn Ziyaad al-Qattwaan ametuzindua: Muhammad bin Ismaa´iyl at-Tirmidhiy ametuhadithia… Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Wasimulizi wake ni wenye kuaminika na wenye kutambulika. Baada ya kutaja masimulizi yote mawili ya Nu´aym bin Hammaad mtunzi amesema ”yote mawili yamesihi kutoka kwake”.
[4] Yamesemwa na Abul-Qaasim al-Baghawiy na Ibn ´Adiy. Maoni sahihi ni mwaka wa 228, kama ilivyo katika “at-Tahdhiyb”.
[5] Bi maana katika ”as-Swahiyh” yake, hata hivyo pamoja na wengine, kama alivoyasema hayo wazi mtunzi katika “Miyzaan-ul-I´tidaal”. Kwa sababu kuna wengi ambao wamemdhoofisha juu ya kumbukumbu yake, na kwa ajili hiyo Haafidhw Ibn Hajar amesema:
”Alikuwa mkweli, lakini mwenye kukosea sana.” (Taqriyb-ut-Taqriyb)
[6] Mtunzi amesimulia kwa cheni ya wapokezi wake mpaka kwa ´Abbaas bin Dahqaan, lakini sikupata wasifu wake.
[7] Imekuja namna hii katika toleo lililochapishwa. Marekebisho yanatokana na maandishi ya vitabu na vitabu vya wasifu.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 171-173
- Imechapishwa: 19/01/2026
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 171-173
Imechapishwa: 19/01/2026
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/152-popote-mnapokuwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket