al-´Ayyaashiy amesema:
”´Abdul-A´laa ameeleza kwamba Abu ´Abdillaah kuhusiana na maneno Yake Allaah:
خُذِ الْعَفْوَ
”Shikamana na usamehevu… ”
“Bi maana uongozi.”
وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ
”… na amrisha mema na jiepushe na wajinga.”[1]
“Kwa maana uongozi.”[2]
Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah, mwarabu anayetokana na kabila la Haashim, kutokana na uongo huu na kiwango cha chini cha kuipotosha Qur-aan. Maneno haya na mengine yanayodaiwa kuwa yake ni miongoni mwa uongo wa Raafidhwah wa Baatwiniyyah.
Maana ya Aayah hii ni kuu sana na yenye adhama kubwa kwa sababu ni maneno ya Mola wa walimwengu na yanalingana na ukubwa wa Qur-aan na adhama ya yule aliyetumwa nayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na ujumbe wake mtukufu. Allaah anamuelekeza Mtume wake mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Aayah hii tukufu awaamrishe watu mema, kwa maana awaamrishe kumwabudu Yeye pekee, kumtakasia matendo Yeye pekee kwa namna ya kumtii kwa kutekeleza amri Zake zote na kujiepusha na makatazo na maonyo Yake. Pia anamwelekeza kushikamana na tabia bora kama subira, upole na kusamehe. Hakika hajiepushi na watu wapumbavu isipokuwa tu yule aliyepambwa na tabia hizi za hali ya juu. Aidha ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameamrishwa kushikamana na yote yaliyomo ndani ya Aayah hii tukufu.
Kisha imani za hawa wapumbavu Raafidhwah zinawasukuma katika tafsiri potofu kama hizi ambazo zinawakilishwa na al-´Ayyaashiy, ambaye upofu wake wa kiakili na upotovu wa fikira umemzuia kutambua ukubwa wa Qur-aan na maajabu ya maana zake.
[1] 7:199
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/43).
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 213
- Imechapishwa: 17/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)