54 – ´Abdul-Maalik bin al-Maajashuun (a.f.k. 214), mwanachuoni wa Madiynah
212 – Ibn Abiy Haatim amesema: Yahyaa bin Zakariyyaa bin ´Iysaa ametuhadithia: Haaruun bin Muusa al-Farawiy ametuhadithia:
”Sikuwahi kusikia mijadala kuhusu Qur-aan mpaka mwaka wa 209. Lililkuja kundi la watu kwa ´Abdul-Maalik bin al-Maajashuun na kuzungumza naye, ambapo akawakemea. Miongoni mwa mambo aliyowaambia: ”Je:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ
“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[1]
ni kiumbe?” Kisha akasema: “Lau ningempata Bishr al-Mariysiy, basi ningemkata shingo yake.”[2]
´Abdul-Maalik alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watukufu wa Maalik. Baba yake ´Abdul-´Aziyz bin al-Maajashuun alikuwa akitoa fatwa pamoja na Maalik katika serikali ya al-Mahdiy. ´Abdul-Malik alifariki mnamo 214.
213 – Abul-Hasan Muhammad bin al-´Attwaar amesema: Nimemsikia Muhammad bin Musw´ab al-´Aabid akisema:
“Yeyote anayesema eti Wewe huongei wala kuonekana Aakhirah, basi ni mwenye kukanusha uso Wako. Nashuhudia ya kwamba uko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu saba, si kama wanavyosema maadui Zako mazanadiki.”[3]
Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad na Abu al-Hasan al-Daraaqutwniy.
214 – al-Marruudhiy amesema[4]: Nimemsikia Abu ´Abdillaah al-Khaffaaf akisema:
”Nimemsikia Ibn Mus’ab akisoma:
عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا
”Hapana shaka Mola wako atakuinua cheo kinachosifika.”[5]
“Ndiyo, atamkalisha pamoja Naye juu ya ´Arshi.”
Imaam Ahmad amemtaja Muhammad bin Mus´ab na akasema:
“Nimeandika kutoka kwake na ni mtu bora kiasi gani!”
Ama kuhusu suala la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuketi juu ya ´Arshi hakuna maandiko yaliyothibiti katika hilo. Bali ipo Hadiyth nyonge juu ya suala hilo[6].
[1] 112:1
[2] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ibn Abiy Haatim ameandika wasifu wa huyu Ibn ´Iysaa na akasema:
”Nimeandika kutoka kwake pamoja na baba yangu. Naye ni mkweli na mwenye kuaminika.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (4/2/146))
Wasifu wa al-Farawiy umeandikwa katika “at-Tahdhiyb”.
[3] as-Sunnah, uk. 34. al-Khatwiyb ameipokea kupitia kwa ad-Daaraqutwniy kisha akasimulia kwamba Ibn Sa´d amesema:
“Abu Ja´far Muhammad bin Mus´ab alikuwa ni msomaji wa Qur-aan, alizisikia Hadiyth na akaketi na watu. Alikuwa – Allaah akitaka – mwenye kuaminika. Alifariki mnamo 228 huko Baghdaad.” (Taariykh Baghdaad (3/280))
Huyu sio Muhammad bin Mus´ab al-Qarqasaaniy.
al-Khatwiyb ameandika wasifu wa Muhammad bin al-´Attwaar na akapokea ya kwamba ´Abdullaah bin Ahmad amesema kwamba alikuwa “mwenye kuaminika” (Taariykh Baghdaad (3/203-204)).
Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Mtunzi pia ameisahihisha katika ufupisho wake.
[4] Katika toleo fupi kurejelewe ”Fadhwiylat-un-Nabiy”.
[5]17:79
[6] Hata hivyo ni kwamba Hadiyth Swahiyh inasema kwamba cheo chenye kusifiwa ni ule uombezi mkubwa wa Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambao ni maalum kwake.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 169-171
- Imechapishwa: 19/01/2026
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 169-171
Imechapishwa: 19/01/2026
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/151-juu-ya-arshi-yake-hali-ya-kuwa-ametengana-na-viumbe-wake/