151. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na nne wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

”Himraan ameeleza kwamba Abu Ja´far amesema kuhusiana na maneno Yake Allaah:

وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ

”Na katika Tuliowaumba kuna ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanahukumu kiadilifu.”[1]

 “Ni maimamu.” Muhammad bin ´Ajlaan ameeleza kwamba amesema: ”Ni sisi.”[2]

Ummah huu uliotajwa katika Aayah hii ni ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao viongozi wake ni Maswahabah wake wema, wakiongozwa na makhaliyfah wanne waongofu Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Allaah aliwaongoza kupitia wao mataifa na watu wengi na wakaijaza dunia kwa uadilifu, wakaamrisha kufanya mema na kukataza maovu. Ahadi ya Allaah ilitimia kupitia wao katika maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Allaah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi – kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao – na atawamakinishia dini yao aliyowaridhia na atawabadilishia amani badala ya khofu yao – [kwa sharti] wananiabudu Mimi na hawanishirikishi na chochote na yeyote atakayekufuru baada ya hapo, basi hao ndio mafasiki.”[3]

[1] 7:181

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/42).

[3] 24:55

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 212-213
  • Imechapishwa: 17/02/2025