Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
123 – Ee Allaah! Wewe unayelinda Uislamu na waislamu! Tuthibitishe juu ya Uislamu mpaka pale tutapokutana Nawe tukiwa nao!
MAELEZO
Haya ni miongoni mwa maneno mazuri ya mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah). Baada ya yeye kutaja masuala haya makubwa na ya khatari, akamuomba Allaah amfanye imara asimpotoshe pamoja na watu wenye mapote na fikira potofu. Hayo yanajulisha uelewa na hekima yake. Mtu asidanganyike na matendo na akadai eti anatambua Tawhiyd na ´Aqiydah na kwamba hakuna juu yake khatari yoyote. Hiyo ni ghururi. Ni juu yake kuogopa mwisho mbaya na kupotea. Ni watu wangapi walikuwa kati na kati wamepotea! Khaswa pale ambapo fitina imekolea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Harakieni matendo kabla ya fitina kubwa kama mfano kipande cha usiku wenye giza kubwa. Mtu anaamka asubuhi akiwa ni muumini na anafika jioni akiwa ni kafiri, anafika jioni akiwa ni muumini na anaamka asubuhi akiwa ni kafiri. Anaiuza dini yake kwa ajili ya mapato ya kidunia.”[1]
Kwa hivyo usisemi eti hauko khatarini na kwamba eti unajua na kuwa eti unaswali. Ni kweli kwamba unaswali na unajua, lakini uko khatarini. Unatakiwa kuogopa. Je, wewe ni bora kuliko Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:
رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ
“Ee Mola wangu! Ufanye mji huu uwe wa amani na unikinge mimi na wanangu kuabudu masanamu.” Ee Mola wangu! Hakika hao wamepoteza wengi kati ya watu”[2]?
Ibraahiym alichelea juu ya nafsi yake kuyaabudu masanamu licha ya kuwa yeye ndiye aliyavunja kwa mkono wake ambapo akaadhibiwa na kutwezwa kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Hakusema kuwa haogopi. Bali alimuomba Allaah amkinge yeye na wanawe kuyaabudia masanamu. Hiyo ina maana kuwa mtu anatakiwa daima kumuogopa Mola wake (´Azza wa Jall). Ni wangapi waliokuwa wameongoka wamepotea! Ni wangapi waliokuwa wamenyooka wamepinda! Ni waumini wangapi wamekufuru na kuritadi! Ni wangapi waliokuwa wamepotea wameongozwa na Allaah! Ni wangapi waliokuwa wamekufuru wameingia katika Uislamu! Jambo liko mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1]Muslim (186).
[2]14:35-36
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 159-161
- Imechapishwa: 25/11/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 159-161
Imechapishwa: 25/11/2024
https://firqatunnajia.com/150-usidanganyike-na-matendo-yako/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)