52 – Yahyaa bin Yahyaa an-Naysaabuuriy (a.f.k. 226), mwanachuoni wa mashariki
208 – Ibn Mandah amesema: Muhammad bin Ya´quub ash-Shaybaaniy ametuzindua: Muhammad bin ´Amr bin an-Nadhwr ametuhadithia: Yahyaa bin Yahyaa ametuhadithia:
”Tulikuwa kwa kwa Maalik wakati ambapo alikuja bwana mmoja na kusema: ”Ee Abu ´Abdillaah!
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”
Amelingana juu vipi?” Maalik akainamisha kichwa chake mpaka akaanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Kulingana si kitu kisichofahamika. Namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mzushi.” Kisha kaamuru atolewe nje.”[1]
209 – Ibn Abiy Haatim amesema: Nimemsikia Muslim bin al-Hajjaaj: Nimemsikia Yahyaa bin Yahyaa akisema:
“Yeyote anayedai kuwa kuna Aayah yoyote ndani ya Qur-aan, kuanzia mwanzo hadi mwisho wake, ambayo ni kiumbe, basi yeye ni kafiri.”
Yahyaa bin Yahyaa alikuwa mtu wa hali ya juu katika umadhubuti, uchaji na utukufu huko Naysaabuur. Ni mara chache macho kuona mtu mfano wake. Alipokea elimu kutoka kwa Maalik, Khariyjah bin Mus’ab na wanazuoni wengine wakubwa. Alifariki mwaka wa 226.
53 – Hishaam bin ´Ubaydillaah ar-Raaziy (a.f.k. 221), mwanachuoni wa Rayy
210 – Ibn Abiy Haatim amesema: ´Aliy bin al-Hasan bin Yaziyd as-Sulamiy ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisema:
”Kuna bwana mmoja alifungwa kwa sababu ya kuwa na ´Aqiydha ya Jahmiyyah. Baadaye akatubu. Kisha mtu huyo akaletwa kwake ili ampe mtihani. Hishaam akamwambia: “Je, unashuhudia ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake hali ya kutengana mbali na viumbe Vyake?” Mtu huyo akasema: “Sijui nini maana ya kuwa mbali na viumbe Vyake.” Ndipo Hishaam akasema: “Mrudisheni gereza. Bado hajatubu.”[2]
Hishaam bin ´Ubaydillaah alikuwa mmoja wa maimamu wa Fiqh katika madhehebu ya Abu Haniyfah. Alijifunza elimu ya Fiqh kutoka kwa Muhammad bin al-Hasan. Alikuwa na heshima kubwa na nafasi ya juu sana katika mji wake. Alifariki mwaka wa 221.
211 – Ibn Abiy Haatim amesema: Abu Haaruun Muhammad bin Khalaf al-Jazzaar[3] ametuhadithia: Nimemsikia Hishaam bin ´Ubaydillaah akisema:
”Qur-aan ni maneno ya Allaah na si kiumbe.” Bwana mmoja akasema: ”Allaah si anasema:
مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ
“Hakuna ukumbusho wowote ule mpya unaowajia kutoka kwa Mola wao… “[4]?
Akasema: ”Ni yenye kuzuka kwetu, kwa Allaah si mpya.”
Kwa sababu ni katika ujuzi Wake – na ujuzi Wake ni wa milele. Amewafundisha waja Wake kutoka humo. Amesema (Ta´ala):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَّمَ الْقُرْآنَ
”Mwingi wa rehema, amefundisha Qur-aan.”[5]
Hivyo mwalimu wa Qur-aan anaweza kuwafundisha watu mia moja au mia mbili kumaliza kuisoma Qur-aan na kuihifadhi na asipoteze kitu katika Qur-aan hiyo. Kama taa inavyoangazia taa nyingine, ambapo taa ya kwanza haibadiliki.
[1] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/305-306). Wasimulizi wake ni wenye kuaminika, mbali na huyu Ibn-un-Nadhwr ambaye simfahamu. Muhammad bin Ya´quub ash-Shaybaaniy ni Haafidhw Ibn-ul-Akhram, mwanachuoni wa Hadiyth wa Naysaabuur na ni miongoni mwa waalimu wa al-Haakim. Alifariki mwaka wa 344. Ibn Mandah ni Haafidhw Muhammad bin Ishaaq.
[2] Simjui Aliy bin al-Hasan bin Yaziyd as-Sulamiy na baba yake. Ibn Abiy Haatim hakuwataja katika ”al-Jarh wat-Ta´diyl”. Kupitia kwake al-Harawiy amemtaja katika ”Dhamm-ul-Kalaam” (1/120 – mswada).
[3] Imekuja namna hii al-Jazzaaz. Ibn Abiy Haatim amesema:
“Muhammad bin Khaalid Abu Haaruun al-Kharraaz ar-Raaziy… Nimeandika kutoka kwake pamoja na baba yangu na Abu Zur´ah. Alikuwa ni mkweli.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (3/2/245))
Inaonekana ndiye huyu. Kwa maana nyingine ni kwamba kile kilichopo katika matoleo ya kuchapishwa na maandishi ya mkono ”Khalaf” ni kosa la uchapaji badala ya ”Khaalid” – na Allaah ndiye anayejua zaidi.
[4] 21:2
[5] 55:1-2
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 168-169
- Imechapishwa: 19/01/2026
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 168-169
Imechapishwa: 19/01/2026
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/150-afukuzwe-kutoka-kwenye-darsa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket