Swali 15: Je, katika kusimamisha hoja ni sharti kuelewa hoja kwa uelewa ulio wazi kabisa au inatosha tu kusimamisha hoja? Tunatarajia maelezo kwa kina pamoja kututajia dalili.
Jibu: Ni wajibu kusimamisha hoja kwa mwenye kuwa na shubuha. Vivyo hivyo mshirikina pindi hoja inapokuwa imesimamishwa dhidi yake, basi udhuru wake unakuwa umeondoka, kwa maana kwamba hoja imemfikia na anajua kuwa jambo hili lina dalili kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haishurutishwi kwamba afahamu hoja kwa namna iliyotajwa. Allaah ametufahamisha kuwa washirikina wamesimamishiwa hoja, licha ya kwamba hawakuielewa kwa uelewa ulio wazi. Hata hivyo hoja imewasimamia kwa kule kuwafikia. Qur-aan imeteremka, wakaisikia na mwonyaji (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwajilia na akawaonya, lakini wakaendelea na ukafiri wao. Kwa hivyo hawakupata udhuru wowote. Kwa ajili hiyo Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا
”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.”[1]
Wamejiliwa na Mtume. Amesema (Ta´ala):
وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ
“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[2]
Hii ni kwa kauli ya Allaah Ta´ala:
Hivyo basi katika kusimamisha hoja sharti ni kufikisha ujumbe. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake! Hakuna yeyote katika ummah huu, si myahudi wala mnaswara, ambaye atasikia juu yangu na asiniamini isipokuwa ataingia Motoni.”
Amesema (Ta´ala) akiwaeleza makafiri:
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa asiyesikia ila wito na kelele tu [za wanyama anaowachunga]; viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[3]
Pamoja na hivo hoja imewasimamia. Allaah amekhabarisha kwamba mfano wao ni mfano wa anayesikia sauti bila kuelewa maana yake, kama mifugo inayosikia sauti ya mchungaji anapowaita, lakini licha ya hio hoja imesimamishwa dhidi yao. Amesema (Ta´ala):
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ
”Haiwi kwa Allaah awapotoze watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie ya kujikinga nayo.”[4]
Hakusema:
”… mpaka ibainike.”
Bali amesema:
حَتَّى يُبَيِّنَ
“… mpaka abainishiwe.”
Huku ndio kusimamisha hoja. Kwa hivyo pindi mtu anapofahamu haki, akatambua dalili na akajua hoja imekuwa wazi kwake, basi hoja imesimamishwa dhidi yake hata kama hajaielewa kwa kina. Kwa kifupi ni kwamba si sharti kuielewa kwa ukamilifu. Hivo ndivo zinavyojulisha dalili na ndio ambayo yamethibitishwa na wanazuoni.
[1] 17:15
[2] 06:19
[3] 02:171
[4] 09:115
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 37-40
- Imechapishwa: 06/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 37-40
Imechapishwa: 06/01/2026
https://firqatunnajia.com/15-namna-mtu-anavyosimamishiwa-dalili-na-hoja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket