58 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: Ahmad bin Sulaymaan al-´Abbaadaaniy ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad bin Harb al-´Abbaadaaniy ametukhabarisha huko ´Abbaadaan: Nimemsikia Bishr bin al-Haarith akisema:

”Hakika fadhilah ya elimu ni kule kuifanyia kazi. Kisha baada ya hapo ikampandisha.”

59 – Abul-Qaasim ´Ubaydullaah bin ´Abdillaah bin al-Husayn al-Khaffaaf ametukhabarisha: Abu Twaalib Muhammad bin Ahmad bin Ishaaq bin al-Buhluul al-Qaadhwiy ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn bin Hamduuyah al-Harbiy ametuhadithia: Nimemsikia Ya´quub bin Shawwaal akisema: Nimemsikia Bishr bin al-Haarith akisema:

”Elimu ni pambo kwa yule mwenye kuifanyia kazi. Ni madhara makubwa yaliyoje kwa yule asiyeifanyia kazi! Ni hoja.”

Akikusudia dhidi ya yule mwenye kujua.

60 – Muhammad bin Ahmad bin Rizquuyah ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad bin Nuswayr al-Khuldiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah al-Hadhwramiy ametuhadithia: ´Abbaas al-´Anbariy ametuhadithia: ´Abdus-Swamad amenihadithia: Nimemsikia Sa´iyd bin ´Utwaarid, ambaye alilia mpaka akaaga dunia, akisema:

”´Iysaa bin Maryam alisema: ”Mpaka lini mtaieleza njia ya kutanga-tanga usiku na hali mnaishi kati ya watu waliochanganyikiwa? Kinachohitajika katika elimu ni kidogo na kinachohitajika katika matendo ni kingi.”

61 – al-´Alaa bin Hazm al-Andalusiy amenihadithia: Muhammad bin al-Husayn bin Baqaa’ al-Miswriy ametukhabarisha: Baba yangu ´Abdul-Ghaniy bin Sa´iyd al-Azdiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ja´far bin al-Ward ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad bin ´Abdis-Salaam ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdullaah bin Ahmad bin Shabbuuyah al-Marwaziy akimnukuu baba yake, ambaye amesema: Nimemsikia Hafsw bin Humayd akisema:

”Niliingia kwa Daawuud at-Twaa-iy, bwana mmoja aliye mkarimu, nikimuuliza juu ya jambo. Akasema: ”Unasamaje juu ya mpiganaji vita anayetaka kutoka kwenda kupigana? Je, si hukusanya zana zake? Atapigana lini ikiwa atayamaliza maisha yake yote kwenye zana? Hakika matendo ndio zana ya matendo. Ni lini atafanya matendo ikiwa atayamaliza maisha yake yote katika kuikusanya?”

62 – Ahmad bin al-Husayn at-Tawwaziy amenikhabarisha: Abu ´Umar Ahmad bin Muhammad bin Muusa bin al-´Allaaf ametukhabarisha: Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: Muhammad bin Abiy ´Umar ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema:

”´Abdullaah alinisikia nikiwasikitikia baadhi ya Mashaykh, ambapo akanambia: ”Ee Abu ´Ubayd, pasi na kujali ni elimu gani uliyokosa, hakikisha usikose kufanya matendo.”

63 – Abiyl-Qaasim ´Ubaydullaah bin Ahmad bin ´Uthmaan as-Swayrafiy ametukhabarisha: Sahl bin Ahmad ad-Diybaajiy ametukhabarisha: Muhammad bin Muhammad bin al-Ash´ath al-Kuufiy ametuhadithia huko Misri: Muusa bin Ismaa´iyl bin Muusa bin Ja´far bin Muhammad ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ´Aliy bin Husayn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy, ambaye amesema:

”Mwenye kuipa nyongo dunia kwetu sisi ni yule mwenye kujua akatendea kazi na yule mwenye kuyakinisha akashika tahadhari. Akifikiwa na jioni katika hali nztio, humshukuru Allaah, na akipambaukiwa katika hali nyepesi, humshukuru Allaah. Huyu ndiye mwenye kuipa kisogo dunia.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 43-45
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy