Muislamu anapaswa kuchinja Udhhiyah kwa niaba yake na familia yake. Awashirikishe katika thawabu za Udhhiyah ili apate ujira mkubwa kwa kutekeleza amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwa kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alichinja kwa niaba yake na familia yake.
Katika Udhhiyah pia kuna kuhuisha Sunnah ya baba yetu Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuna kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa kumwaga damu, pamoja na kupanua hali ya furaha kwa familia na masikini katika siku ya ´Iyd na kuwapelekea zawadi ndugu wa karibu na majirani.
Kumchinja mwenyewe mnyama wa Udhhiyah ni bora kuliko kutoa swadaqah ya thamani yake, kwa sababu ndani ya Udhhiyah kuna kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kuchinja kwa ajili Yake, kuna kuonyesha alama za Dini Yake pamoja na faida nyingine nyingi ambazo ni bora kuliko kutoa pesa kama swadaqah.
Kwa kuwa lengo la Udhhiyah ni kuchinja kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall), basi inapendelewa kwa mtu kumchinja mwenyewe mnyama wake wa Udhhiyah nyumbani kwake na ale sehemu ya nyama hiyo na awalishe wengine.
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kuhusu kichinjwa cha Hadiy:
فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ
“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”[1]
Mkusudiwa ni yule mwenye uhitaji mkubwa kabisa na hana chochote.
Kwa msingi huu, sioni kuwa ni bora kupeleka fedha nchi nyingine ambako kuna uhitaji zaidi, ili ichinjwe Udhhiyah kwa niaba yake huko, kwa sababu mbili:
1 – Udhhiyah ni alama ya dini inayomhusu binafsi muislamu. Kuchinja mwenyewe nyumbani kunafufua alama hiyo ya dini, huleta furaha kwa familia na watoto. Lakini yanakosekana mambo haya kwa kutuma pesa nchi nyingine.
2 – Inawezekana kwa mtu mwenye uwezo akatuma pesa, chakula, mavazi au mfano wa hayo katika nchi aliyokusudia. Pengine faida yake inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko nyama ya Udhhiyah.
[1] 22:28
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 22-23
- Imechapishwa: 11/05/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 22-23
Imechapishwa: 11/05/2025
https://firqatunnajia.com/15-mapendekezo-kuhusu-mnyama-wa-udhhiyah/