121 – Duhaym ametukhabarisha: Muhammad bin Shu´ayb ametukhabarisha: adh-Dhwahhaak bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Hawshab ametukhabarisha:

“Bwana mmoja alimwendea Ibn Abiy Zakariyyaa na akasema: “Unasemaje ikiwa mtu fulani ataingia nyumbani kwa mwanamke fulani?” Akasema: “Halali na jambo zuri.” Bwana yule akasema: “Alikuwa na mtu pamoja naye.” Ndipo Ibn Abiy Zakariyyaa akasema: “Hakika sisi ni wa Allaah! Umemfikiria hivo ndugu yako. Inatia aibu kuniambia jambo kama hilo.” Walipokaribia msikitini akasema: “Hapana, naapa kwa Allaah! Huingii ndani mpaka urudi na utawadhe kutokana na uliyoyasema.”

122 – Abu Bakr ametukhabarisha: Shariyk ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Ishaaq, ambaye amesema:

“Abu Swaalih alisoma mstari wa shairi la kejeli, ambapo akaomba maji na kusukutua kinywa chake.”

123 – Abu Mas´uud ametukhabarisha: Mu´aawiyah bin ´Amr ametukhabarisha, kutoka kwa Zaa’idah, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, ambaye amesema:

“Kunatawadhiwa baada ya hadathi na kuwaudhi waislamu.”

124 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Aaswim bin Abiyn-Najuud, kutoka kwa Dhakwaan Abu Swaalih, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye amesema:

“Mmoja wenu anatawadha kwa chakula cha halali lakini hatawadhi kwa neno baya analolisema?”

125 – Ayyuub al-Wazzaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Sulaym ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Amr, kutoka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Shamr, ambaye amesema:

“Abu Swaalih alitusomea mistari michache ya mashairi. Ulipofika wakati wa swalah, Abu Swaalih akasimama na kutawadha. Nikasema: “Kwa nini unatawadha?” Akasema: ”Kutokana na maneno niliyoyasema.”

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 30/06/2025