Nia katika ´ibaadah zote mahali pake ni moyoni. Kwa msemo mwingine haijuzu kuitamka kwa sauti, kwa sababu hilo halikupokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah wake kwamba walikuwa wakisema:

”Nimekusudia kufunga.”

”Nimekusudia kuswali.”

Kwa hiyo kuitamka nia kwa sauti ni Bid´ah iliyozuliwa. Inatosha katika nia kula na kunywa kwa kusudia kufunga. Shaykh Taqiyy-ud-Diyn Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yeye anapokula chakula cha usiku anakula chakula cha mtu anayekusudia kufunga, kwa sababu hiyo hutofautishwa kati ya chakula cha usiku wa ´iyd na chakula cha nyusiku za Ramadhaan.”

Amesema pia:

“Kila anayejua kuwa kesho ni Ramadhaan na anataka kuifunga, basi ameshaweka nia, jambo ambalo ndio kitendo cha waislamu wengi.”

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 22
  • Imechapishwa: 05/02/2026