Ufupisho ni kwamba kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pasi na kujali aina na sura mbalimbali zinazotumiwa katika kufanya hivo, ni jambo la Bid´ah na ni maovu. Ni wajibu kwa waislamu kulikemea na kukemea Bid´ah nyinginezo. Badala yake wajishughulishe na kuhuisha Sunnah na kushikamana nazo bara bara. Mtu asidanganyike na wale wenye kueneza Bid´ah hizi na kuzitetea. Hakika kufanya hivi kunawafanya watu hawa wanapata uchangamfu wa kueneza Bid´ah zaidi kuliko uchangamfu wanaoupata katika kuhuisha mambo ya Sunnah. Bali huenda wasitilii umuhimu wowote kabisa wa kuhuisha Sunnah. Kwa hivyo haijuzu kumfuata wala kumuiga yule anayeeneza Bid´ah. Haijalishi kitu hata kama wenye kufanya hivo watakuwa ndio wengi. Anayefuatwa na kuigwa ni yule mwenye kufuata mwongozo wa Sunnah katika Salaf na wafuasi wao, ingawa watakuwa wachache wenye kufanya hivo. Kwani haki haijulikani kwa kuwaangalia watu, kinyume chake wenye haki hujulikana kwa kuiangalia haki. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika yule atakayeishi kipindi kirefu katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi jilazimisheni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Shikamaneni nazo barabara na ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
Ametubainishia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth hii tukufu ni kina nani tunaotakiwa kuwaiga wakati wa makinzano. Halafu akabainisha kuwa maneno na matendo yote yanayoenda kinyume na Sunnah ni Bid´ah na kwamba kila Bid´ah ni upotevu. Lau tutaangalia sherehe ya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tutaona kuwa hayana msingi katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala katika Sunnah ya makhaliyfah wake waongofu. Kwa hivyo ni katika mambo yaliyozuliwa na ni katika Bid´ah zenye kupotosha. Msingi huu unaopatikana katika Hadiyth hii umefahamishwa na maneno Yake (Ta´ala):
فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[2]
Kurejea kwa Allaah ni kurejea katika Qur-aan, na kurejea kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kurejea katika Sunnah zake baada ya kufa kwake. Quraan na Sunnah ndio marejeo wakati wa kuzozana. Ni sehemu gani katika Quraan na Sunnah kitu kinachofahamisha kuwa inafaa kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
Kwa hiyo ni wajibu kwa yule mwenye kufanya hivo au kuonelea kuwa ni jambo zuri atubie kwa Allaah (Ta´ala) na aachane na hilo na Bid´ah nyinginezo. Hii ndio sifa ya muumini anayetaka haki. Kuhusiana na yule mwenye kufanya ukaidi na jeuri baada ya kuwa hoja imekwishamsimamia, huyo hesabu yake iko kwa Mola Wake.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) aturuzuku kushikamana na Quraan na Sunnah mpaka siku tutakutana Naye.
Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake.
[1] Ahmad (16692) at-Tirmidhiy (2676).
[2] 4:59
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 156-157
- Imechapishwa: 06/09/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 156-157
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/15-kipimo-ni-salaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket