Kumfundisha wanafunzi ni faradhi ya kutoshelezana. Ikiwa hakuna anayefaa isipokuwa mmoja, basi inakuwa wajibu juu yake peke yake. Ikiwa wapo wengi na elimu inapatikana kwa baadhi yao, basi wakikataa wote watapata dhambi. Wakisimama baadhi yao basi jukumu linaondoka kwa waliobaki. Ikiwa ataombwa mmoja wao akakataa, basi maoni yenye nguvu zaidi ni kwamba hapati dhambi. Lakini inachukiza kwake kufanya hivyo ikiwa hana udhuru.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 31
  • Imechapishwa: 26/08/2026