79 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoingia chooni husema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخُبْثِ وَالْخَبائِث

“Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokamana na mashaytwaan ya kiume na ya kike.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Kinachokusudiwa hapa ni kuomba du´aa wakati anapotaka kuingia chooni. Makusudio si kwamba aombe du´aa wakati yuko anakidhi haja. Haifai kumtaja Allaah katika maeneo pa kukidhia haja. Inapendeza kusema anapotaka kuingia chooni:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخُبْثِ وَالْخَبائِث

“Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokamana na mashaytwaan ya kiume na ya kike.”

Ina maana kwamba unaomba kinga, ulinzi na kushikamana na Allaah kutokamana na shari ya mashaytwaan ya kiume na ya kike. Kwa hivyo wewe unajilinda kwa Allaah kutokana na mashaytwaan ya kiume na ya kike.

[1] al-Bukhaariy (6322) na Muslim (275).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 83
  • Imechapishwa: 26/10/2025