72 – ´Ubayd al-Muktib amesimulia kutoka kwa Mujaahid ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Allaah ameumba vitu vinne kwa mkono Wake: Aadam, kalamu, ´Arshi na Pepo ya Edeni. Akaviambia viumbe vyengine vyote: ”Kuwa!” na vikawa.”[1]

73 – Imesihi kwamba ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw amesema:

”Malaika walisema: ”Ee Mola wetu! Miongoni mwetu wako waliokurubishwa, wengine wenye kubeba ´Arshi na wengine ni waandishi watukufu. Umewaumba wanaadamu na ukawapa dunia; nasi tupe Aakhirah.” Akasema: ”Sintofanya kizazi cha ambaye nimemuumba kwa mkono Wangu kuwa kama ambaye nimemuumba kwa kusema ”Kuwa!” na akawa.”

75 – Jaabir ameipokea hiyohiyo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

76 – Imethibiti kwamba Abu Hurayrah amesema:

”Allaah alisema kumwambia Aadam na huku mikono Yake miwili ikiwa wazi: ”Chagua unaotaka.” Akasema: ”Nachagua mkono wa kuume wa Mola wangu.”[2]

77 – Imesihi kwamba al-Mughiyrah bin Shu´bah amesema:

”Muusa alimuuliza Mola wake: ”Ee Mola! Nieleze mtu wa Peponi ambaye yuko na nafasi ya juu kabisa?” Akasema: ”Wale ambao heshima yao Nimeipanda kwa mkono Wangu na nikaipiga muhuri; hakuna jicho limekwishaiona, hakuna sikio limekwishaisikia na wala haijapita kwenye moyo wa yeyote.”[3]

Ameipokea Muslim.

78 – Imesihi kutoka kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa al-Hakiym bin Jaabir ambaye amesema:

”Nimekuelezeni kuwa Mola wenu hakuna kitu alichokigusa kwa mkono Wake isipokuwa vitu vitatu: Alipanda Pepo kwa mkono Wake, akamuumba Aadam kwa mkono Wake na akaandika Tawraat kwa mkono Wake.”

78 – Mfano wa hayo yamesihi kutoka kwa Mughiyth bin Sumayy.

79 – Imesihi kutoka kwa Naafiy´ bin ´Umar al-Jamhiy ambaye amesema:

”Nilimuuliza Ibn Abiy Mulaykah kama Allaah ana mkono mmoja au miwili. Akajibu: ”Miwili.”[4]

Endapo nitazitaja Hadiyth zote zinazotaja mikono miwili ya Allaah, basi kitakuwa kirefu.

[1] al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (693), al-Haakim (2/319), ash-Shariy´ah, uk. 313, na wengineo.

[2] al-Haakim aliyesema:

”Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim.” (al-Mustadrak (1/64))

[3] Muslim (312), at-Tirmidhiy (3198) na al-Bayhaqiy (690).

[4] ar-Radd ´alaa Bishr al-Mariysiy, uk. 38

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 78-81
  • Imechapishwa: 04/06/2024