50 – ´Aaswim bin ´Aliy (a.f.k. 221), mwalimu wa al-Bukhaariy
179 – Tumesimuliwa kwamba ´Aaswim bin ´Aliy bin ´Aaswim al-Waasitwiy amesema:
“Nilijadiliana na Jahm ilidhihirika kutokana na maneno yake ya kwamba haamini kuwa kuna Mola juu ya mbingu.”
´Aaswim alikuwa mwenye kuhifadhi, mwenye elimu iliobobea na mkweli. Alichukua elimu kutoka kwa Shu´bah, Ibn Abiy Dhi’b na wengineo. al-Khatwiyb amesema wakati alipotaja wasifu wake:
”al-Mu’taswim alituma mtu kuhesabu watu walioketi katika halaqa ya ´Aaswim katika msikiti wa Ruswaafah. Alikuwa akiketi juu ya paa la ua na watu umati wa watu ukiwa chini umemzunguka na idadi yao ilikuwa kubwa sana. Siku moja umati wa watu ulikuwa mkubwa mpaka akasema “al-Layth bin Sa’d ametuhadithia” mara kumi na nne, lakini watu hawakuweza kusikia kutokana na wingi wao. Mkusanyaji wa Hadiyth, Haaruun alilazimika kupanda mtende ili kuwasimulia. Watu walikadiriwa kuwa 120 000. Yahyaa bin Ma’iyna amesema: “´Aaswim bin ´Aliy ni bwana wa waislamu.”
Alifariki mwaka mmoja na al-Qa´nabiy.
51 – al-Humaydiy [´Abdullaah bin az-Zubayr] (a.f.k. 219)
207 – Mtunzi wa kitabu amesimulia kutoka kwa ´Abdul-Ghaffaar bin Muhammad: Abu ´Aliy as-Sawwaan ametuzindua: Bishr bin Muusa ametuzindua: al-Humaydiy ametuzindua:
”Misingi ya ´Aqiydah kwetu ni kuamini makadirio, ya kheri na ya shari, machungu na matamu… Vivyo hivyo yale yaliyotamkwa na Qur-aan na Hadiyth, kama vile:
بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ
”Bali mikono Yake imefumbuliwa.”[1]
وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ
“… na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[2]
Na yanayofanana na haya kutoka Qur-aan na Hadiyth. Hatuongezi juu yake wala hatuyafasiri na tunasema. Bali tunasimama pale ambapo Qur-aan na Sunnah zimesimama na tunasema:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]
Yeyote anayedai vinginevyo basi yeye ni mtu wa batili na Jahmiy.”[4]
´Allaamah Abu Bakr ´Abdullaah bin az-Zubayr al-Qurashiy al-Asdiy al-Humaydiy alikuwa, baada ya mwalimu wake Sufyaan bin ´Uyaynah, muftiy na mwanachuoni wa watu wa Makkah. al-Bukhaariy na wakubwa wengine wamehadithia kutoka kwake. Alifariki mnamo 219.
[1] 5:64
[2] 39:67
[3] 20:5
[4] al-Khatwiyb amemweleza Abu Twaahir ´Abdul-Ghaffaar bin Muhammad al-Mu’addib ifuatavyo:
“Nimeandika kutoka kwake. Nimemsikia Abu ´Abdillaah as-Suuriy akimsema vibaya na kwa namna ambayo anaonekana kuwa ni dhaifu.” (Taariykh Baghdaad (11/116))
Pengine alifanyiwa ufuatiliaji, kwani nimemuona Ibn Taymiyyah akithibitisha maneno haya kutoka kwa al-Humaydiy katika kitabu chake “Mufasswal-ul-I´tiqaad”, uk. 6 – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 167-168
- Imechapishwa: 19/01/2026
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 167-168
Imechapishwa: 19/01/2026
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/149-anayesema-vingine/