al-´Ayyaashiy amesema:
”Sulaymaan al-Labbaan amesema: ’Abu Ja´far alisema: “ Je, unajua mfano wa al-Mughiyrah bin Shu’bah? Akasema: ”Hapana” Akasema: ”Mfano wake ni kama wa Bal’am ambaye alilitambua jina kuu la Allaah. Allaah amesema juu yake:
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ
“Wasomee habari za yule Tuliyempa Aayah Zetu akajivua nazo. Shaytwaan akamfuata na [hatimaye] akawa miongoni mwa waliopotoka.”[1][2]
Allaah amtakase Abu Ja’far kutokana na uongo huu. Nyinyi ndio mnafaa zaidi kutuhumiwa kwa maneno haya ambayo mnamnasibishia al-Mughiyrah (Radhiya Allaahu ´anh). Hakika alikuwa miongoni mwa Maswahabah watukufu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Msimamo wake Hudaybiyyah unajulikana. Msimamo wake dhidi ya mababu zenu wafursi unatambulika. al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Ziyaad bin Jubayr, kutoka kwa Jubayr bin Hayyah ambaye amesema:
”´Umar alituchagua na akamteua an-Nu´man bin Muqrin kuwa kiongozi wetu. Tulipofika katika ardhi ya adui, kiongozi wa Kisraa alitoka akiwa na watu 40.000. Mkalimani akasimama na kusema: “Naombeni mtu mmoja azungumze nami.” al-Mughiyrah akasema: “Uliza unachotaka.” Mkalimani akasema: “Nyinyi ni akina nani?” al-Mughiyrah alijibu: “Sisi ni watu wa kiarabu tulioishi maisha ya taabu na shida kubwa. Tulikuwa tunakula ngozi na kokwa za mitende kutokana na njaa, tukavaa manyoya na ngozi za wanyama na tunaiabudu miti na mawe. Tulipokuwa katika hali hiyo, Mola wa mbingu na ardhi (Ta´ala) akatutumia Mtume anayetokana nasi, ambaye tunamjua baba na mama yake. Mtume wetu na Mola wetu wakatuamrisha tuwapige vita mpaka mumwabudu Allaah peke yake au mlipie kodi ya kulindwa. Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatufahamisha kutoka katika ujumbe wa Mola wetu ya kwamba atakayekufa miongoni mwetu ataingia Peponi ndani ya neema zisizoelezeka, na yeyote atakayebaki miongoni mwetu atatawala shingo zenu”.”[3]
[1] 7:175
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/42).
[3] al-Bukhaariy (3159).
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 211-212
- Imechapishwa: 17/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)