148. Badilisha ´Aqiydah yako tuendelee kukupa ruzuku?

48 – Imaam al-Qa´nabiy (a.f.k 221)

204 – Banaan bin Ahmad amesema:

”Tulikuwa kwa ya al-Qa´nabiy wakati alipomsikia mtu mmoja katika Jahmiyyah akisema kwamba mwingi wa Rehema ametawala (استولى) juu ya ´Arshi. Ndipo al-Qa´nabiy akasema: “Yeyote asiye na yakini kwamba mwingi wa Rehema amelingana juu juu ya ´Arshiy amestawi kama inavyokubalika katika nyoyo za watu wa kawaida, basi huyo ni Jahmiy.”

Ameipokea ´Abdul-´Aziyz al-Quhaytwiy[1].

Watu wa kawaida hapa wanakusudiwa watu wa kawaida katika wanazuoni, kama nilivyobainisha katika wasifu wa Yaziyd bin Haaruun ambaye ni imamu wa watu wa Waasitw. Hakika al-Qa´nabiy alikuwa ni miongoni mwa maimamu wa uongofu hadi baadhi ya wenye kuhifadhi walimuinua na kumtanguliza mbele ya Imaam Malik. Alifariki mwaka 221 akiwa na zaidi ya miaka 80. Yeye ndiye alikuwa mwalimu mkubwa zaidi wa Imaam Muslim kabisa.

49 – ´Affaan (a.f.k >219), mmoja katika vigogo wa Sunnah.

205 – Ibn Abiy Haatim amesema: Yahyaa bin Zakariyyaa bin ´Iysaa ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Bakr as-Sammaar amenihadithia:

”Nimemsikia ´Affaan bin Muslim, baada ya kutoka katika nyumba ya Ishaaq bin Ibraahiym[2], ambaye alimjaribu kuhusu Qur-aan, akisema: “Amesema: ”Ruzuku yako itaongezwa ikiwa utakubali kuwa Qur-aan ni kiumbe.” Nikasema: ”Najikinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali na rehema za Allaah. Wanataka kuyabadilisha maneno ya Allaah:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliye hai, Anayekisimamia kila kitu.”[3]

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[4]

Je, haya yameumbwa? Nimekutana na Shu´bah, Hammaad bin Salamah na maswahiba wa al-Hasan wakisema: ”Qur-aan ni maneno ya Allah na hayakuumbwa.” Ndipo akasema: ”Basi tunasimamisha ruzuku yako.” Akasema:

وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ

“Na katika mbingu, kuna riziki zenu, na yale mnayoahidiwa.” [5]

Inasemekana kuwa ruzuku yake ilikuwa ni dirhamu elfu moja kwa mwezi. Akayaacha hayo kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Alifariki mwaka wa 219.

[1] Imekuja namna hii katika nakala iliyochapishwa, ilihali katika nakala ya maandishi imeandikwa “al-´Ujayliy.” Haijalishi iwapo ni huyu au yule, bado sijamtambua ´Abdul-´Aziyz huyu. Kisha nikaona al-Quhaytwiy katika toleo fupi lililochapishwa.

Banaan bin Ahmad hana neno na wasifu wake uko katika “Taariykh Baghdaad” (7/100).

[2] Mwanamfalme Ishaaq bin Ibraahiym bin Mus´ab al-Khuzaa´iy, binamu yake na Twaahir bin al-Husayn. Alikuwa meya wa Baghdaad kwa zaidi ya miaka ishirini. Alikufa mnamo 235, kama ilivyokuja katika “ash-Shadhaaraat”.

[3] 3:2

[4] 112:1

[5] 51:22 Yahyaa bin Abiy Bakr as-Sammaar sijamjua mpaka sasa, lakini amefanyiwa ufuatiliaji kupitia njia zingine. Abu Zakariyyaa Yahyaa bin Zakariyyaa bin ´Iysaa al-Marwaziy alikuwa mkweli na mwenye kuaminika, kama alivosema Ibn Abiy Haatim (4/2/146). al-Khatwiyb amepokea masimulizi haya katika “Taariykh Baghdaad (12/270-271) chini ya wasifu wa ´Affaan pasi na sentesi ”Nimekutana na Shu´bah… .” Cheni ya wapokezi ni yenye nguvu.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 166-167
  • Imechapishwa: 09/01/2026
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy