al-´Ayyaashiy amesema kuhusiana na:
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ
“Pindi Mola wako alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao [na akawauliza]: “Je, Mimi siye Mola wenu?”[1]
“Ibn Miskaan ameeleza kutoka kwa baadhi ya marafiki zake ambao wamesimulia kwamba Abu Ja´far amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Ummah wangu ulionyeshwa kwangu wakati wa fungamano. Mtu wa kwanza kuniamini alikuwa ni ´Aliy. Yeye ndiye alikuwa wa kwanza kunisadikisha wakati nilipotumwa. Yeye ndiye mkweli mkubwa (الصديق الأكبر) na ndiye mpambanuzi (الفاروق) ambaye anapambanua kati ya haki na batili.”[2]
Malengo ya uongo huu ni kuficha ile sifa ya kipekee aliyosifika nayo Abu Bakr, ambaye ndiye mkweli mno wa wakweli, na pia kuficha ile sifa ya kipekee aliyosifika nayo ´Umar, ambaye ndiye mwenye kupambanua kati ya haki na batili. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waumini ndio waliowasifu hivo. Waongo wameongeza upokezi kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) unaosema:
“Kipindi hicho Allaah aliwazungumzisha watu wa fungamano ambapo na wao wakazungumza Naye. Akawaambia: “Hakika mimi ndiye Allaah, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.” Wakakiri kumtii na uola Wake, na Akawapambanua Mitume, Manabii na wasii na akawaamrisha viumbe kuwatii. Wakayakubali hayo katika fungamano.”
Kwa hivyo madhehebu ya Raafidhwah yalithibitishwa tokea wakati huo? Ina maana kwamba watu wanalazimika kuyaamini? Allaah awaue waongo. Tazama na ulinganishe maneno Yake:
أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ
“Je, Mimi siye Mola wenu?”
na maneno yao:
“Hakika mimi ndiye Allaah, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”
uone namna ambavyo Raafidhwah Baatwiniyyah wana urahisi katika kusema uongo na kupotosha.
[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/41).
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/41).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 209-210
- Imechapishwa: 19/09/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 209-210
Imechapishwa: 19/09/2018
https://firqatunnajia.com/148-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-kumi-na-moja-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)