146. Mitazamo sampuli tatu juu ya watenda madhambi makubwa

Kwa hivyo watu wamegawanyika makundi matatu kuhusu watenda madhambi makubwa yaliyo chini ya shirki:

1 – Khawaarij na Mu´tazilah ambao wanawatoa nje ya Uislamu. Tofauti ni kwamba Khawaarij wanasema kuwa ni makafiri ilihali Mu´tazilah wanasema kuwa sio waislamu wala sio makafiri.

2 –Murji-ah wanasema kuwa ni waumini wenye imani kamili. Muda wa kuwa wanaamini mioyoni mwao, kama wanavyoonelea wengi wao, na wanatamka kwa ulimi wao, kama wanavyoshurutisha wengine, wanaona kuwa ni waumini wenye imani kamili. Wanaona kuwa madhambi, ijapo yatakuwa makubwa, hayaipunguzi imani. Fikira hii ni upotofu pia.

3 – Haki –ni ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mtenda dhambi kubwa sio kafiri muda wa kuwa dhambi yake ni chini ya shirki. Hata hivyo imani yake ni pungufu. Ni wajibu kujua jambo hili. Ni lazima kuliweka hilo akilini mwako. Leo waovu yamezidi maovu yao. Wameanza kudhihirisha ´Aqiydah ya Murji-ah ili kuieneza kati ya watu na kuficha upotofu wao nyuma yake. Mwanafunzi kuyajua mambo haya ni miongoni mwa mambo ya wajibu kabisa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 24/11/2024