al-´Ayyaashiy amesema:
“Zaadhaan ameeleza kutoka kwa Salmaan: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimwambia ´Aliy zaidi ya mara ishirini: “
“Ee ´Aliy! Hakika wewe na wasii baada yako ndio watakaosimama kati ya Pepo na Moto. Hakuna yeyote atakayeingia Peponi isipokuwa yule aliyekutambueni na nyinyi mkamtambua, hakuna yeyote atakayeingia Motoni isipokuwa yule aliyekukanane na nyinyi mkamkana.”[1]
Huu ni uzushi. Mwandishi ni Baatwiniy na anamsemea sana uongo Allaah na Kitabu Chake. Cheni ya wapokezi kutoka kwake mpaka kwa Zaadhaan ina watu wasiojulikana. Hata kama Zaadhaan alikuwa mwaminifu, basi itambulike kuwa alikuwa Shiy´iy na alikuwa akisimulia Hadiyth pasi na Maswahabah katika cheni ya wapokezi. Katika hali hii akifikia mpaka kupokea kitu kinachosapoti Bid´ah yake. al-´Ayyaashiy amesema:
وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ
”Baina yao ni kizuizi, na katika al-A’raaf patakuweko watu wanaowatambua wote kwa alama zao.”[2]
“Sa´d bin Twarif amesimulia kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema kuhusiana na Aayah hiyo: “Ee Sa´d! Hicho ni kizazi cha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna yeyote atakayeingia Peponi isipokuwa yule aliyewatambua na wao wakamtambua, hakuna yeyote atakayeingia Motoni isipokuwa yule aliyewakana na wao wakamkana.”[3]
Katika cheni hii ya wapokezi yupo Baatwiniyyah ambaye ni al-´Ayyaashiy. Kati yake yeye na Sa´d bin Twariyf kuna pengo. Sa´d bin Twariyf alikuwa ni Shiy´iy mwenye kuachwa. Ibn Hibbaan alimtuhumu uzushi. Abu Ja´far ni mwenye kutakasika kutokamana na uzushi huu. Hata kama kweli angelisema hivo, basi sisi hatungelikubali isipokuwa kwa dalili ya wazi, na dalili hakuna.
[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/18).
[2] 07:46
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/18).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 200
- Imechapishwa: 12/09/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 200
Imechapishwa: 12/09/2018
https://firqatunnajia.com/143-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-saba-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)