Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Ni jambo linalotambulika vyema kwa waumini kwamba Allaah amemtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa uongofu na dini ya haki ili iweze kushinda juu ya dini zingine zote.

MAELEZO

Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ

“Yeye adiye aliyemtuma Mtume Wake kwa uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu ya dini zote, japo washirikina watachukia.”[1]

Kwa maan juu ya dini zote, jambo ambalo limetimia. Uislamu umeshinda uyahudi, ukristo na dini zote nyingine ambapo ukaenea mashariki na magharibi na ukashinda kwa hoja, kwa dalili na ubainifu.

Ungofu ni elimu yenye manufaa na dini ya haki ni matendo mema. Katika elimu yenye manufaa ni yale aliyoyataja kuhusu haki ya Allaah ikiwa ni pamoja na kumpwekesha, majina na sifa Zake. Huu ndio msingi wa elimu yenye manufaa ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja nayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja na ubainifu mkamilifu wa kila wanachokihitaji watu katika mambo ya dini yao. Basi inawezekanaje Allaah amemtuma kwa uongofu kisha asiwabainishie watu mada hii?

[1] 9:33

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 229-230
  • Imechapishwa: 16/07/2026