111 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Abiy Marwaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ka´b, ambaye amesema:
“Allaah (Tabaarak wa Ta’ala) anasema: “Mimi hukaa na yule anayenitaja.”
112 – al-Hasan bin as-Sabbaah al-Bazzaar ametukhabarisha: Hajjaaj bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa Sulaymaam bin al-Mughiyrah: Nimemsikia Yuunus bin ´Ubayd akisema:
“Hakuna mtu yeyote anayefikiri kabla ya kusema, isipokuwa utaona matunda ya hayo katika matendo yake mengine.”
113 – al-Hasan bin as-Sabbaah al-Bazzaar ametukhabarisha: Hajjaaj bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa Mubarak bin Fadhwaalah, kutoka kwa Yuunus bin ´Ubayd, ambaye amesema:
“Huwezi kupata wema ambao unafuatwa na wema mwingine wote isipokuwa ulimi. Tunamwona mtu anayefunga sana na baadaye anafunguia haramu, akisimama usiku kucha kuswali na baadaye anatoa ushahidi wa uwongo wakati wa mchana. Hata hivyo humuoni akiongea isipokuwa ya kheri tu na hivyo ukachelea juu yake.”
114 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym at-Taymiy, kutoka kwa al-Haarith bin Suwayd, ambaye amesimulia kuwa ´Abdullaah amesema:
“Ni afadhali nitawadhe kwa maneno machafu kuliko kutawadha kwa chakula cha halali.”
115 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Aaswim bin Abiyn-Najuud, kutoka kwa Dhakwaan Abu Swaalih, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye amesema:
“Mmoja wenu anaweza kutawadha kwa chakula cha halali lakini asitawadhe kwa neno baya analomwambia ndugu yake?”
116 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ibn ´Ulayyah ametukhabarisha, kutoka kwa Ayyuub, kutoka kwa Muhammad, ambaye amesema:
“Nimegundua kwamba mzee mmoja wa Answaar alikuwa akipita kwenye kikao chao na kusema: “Tawadheni upya! Baadhi ya mnayoyasema ni mabaya zaidi kuliko hadathi.”
117 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ibn ´Ulayyah ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad, ambaye amesema:
“Tulimwambia ´Ubaydah: “Ni lini wudhuu´ unachenguka?” Akasema: ”Kutokana na hadathi na kumuudhi muislamu.”
118 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Khaalid al-Ahmar ametukhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin ´Ajlaan, kutoka kwa al-Haarith, ambaye amesema:
“Nilikuwa nimemshika mkono Ibraahiym wakati ambapo nilimsengenya bwana mmoja, ambapo akasema: “Rudi ukatawadhe. Walikuwa wakizingatia hicho ni kitu kisichoepukwa.”
119 – Abu Bakr ametukhabarisha: Humayd bin ´Abdir-Rahmaan ametukhabarisha, kutoka kwa Muusa bin Abiyl-Furaat, ambaye amesema:
“Watu wawili walimuuliza ‘Atwaa’ na wakasema: “Kuna bwana mmoja alipita karibu nasi ambapo tukasema kuwa ana tabia za kike.” Akasema: “Je, mlisema hivo kabla ya kuswali au baada ya kuswali?” Wakasema: “Baada ya kuswali.” Ndipo akasema: “Tawadheni na mswali tena. Kwani hamna swalah.”
120 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Dhamrah bin Rabiy´ah ametukhabarisha, kutoka kwa Rajaa’ bin Abiy Salamah, aliyesema:
”Nilimwambia Mujaahid: ”Ee Abul-Hajjaaj, usengenyi unachengua wudhuu´?” Akasema: ”Ndio, na unaharibu swawm.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 26-28
- Imechapishwa: 30/06/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 26-28
Imechapishwa: 30/06/2025
https://firqatunnajia.com/14-wudhuu-baada-ya-usengenyi-na-matusi/