Kwa Kitabu kilichoteremshwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawatoa watu kutoka katika visa vya ukafiri na shirki na kuwaingiza ndani ya nuru ya imani na Tawhiyd na elimu yenye manufaa. Elimu ni nuru, ujinga ni visa. Kufuru ni viza, imani ni nuru. Shirki ni viza, Tawhiyd ni nuru. Hili ndio lilikuwa jukumu la Mtume; kuwatoa watu kutoka katika viza na kuwaingiza ndani ya nuru. Msingi wa nuru hiyo ni kumtambua Allaah (Jalla wa ´Alaa) kupitia majina na sifa Zake na kumwabudu Yeye pekee, hali ya kuwa hana mshirika. Namna hii ndio kutoka nje ya viza na kuingia ndani ya nuru. Kwa sababu hapo kale watu walikuwa wakiabudia masanamu, mawe na miti. Kila mmoja alikuwa akikiabudu kile kinachompendeza na yale waliyopambiwa na mashaytwaan. Hivi ni viza. Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah. Hii ndio nuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumwa ili awatoe watu kutoka katika viza vya kufuru, shirki na ujinga na kuwaingiza ndani ya nuru ya elimu na yakini, kumtambua Allaah kwa majina na sifa Zake na kumwabudu Yeye pekee:

الر كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ

 “Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[1]

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ

“Allaah ni mlinzi wa wale ambao wameamini; Anawatoa kutoka katika viza na  kuwaingiza katika nuru.  Na wale ambao wamekufuru walinzi  wao ni Twaaghuut; huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza.”[2]

Kuwa na ujinga juu ya Allaah ni katika viza na utambuzi juu ya Allaah ni nuru:

بِإِذْنِ رَبِّهِمْ

”… kwa idhini ya Mola wao… ”

Bi maana kwa Shari´ah na dini Yake. Kuna sampuli mbili za idhini ya Allaah: ya kilimwengu na ya kidini:

إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ

”… waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”

Nayo ni njia ya Allaah. Allaah ndiye Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika. Njia yake ni ile njia inayofikisha Kwake, nayo ni ile Tawhiyd, imani na matendo mema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vinginevyo]; vikakufarikisheni na njia Yake!”[3]

[1] 14:01

[2] 2:257

[3] 6:153

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 28/07/2024