14. Ni ipi hukumu ya mtu anayemuomba asiyekuwa Allaah huku akiishi miongoni mwa waislamu na kwa lugha ya Qur-aan?

Swali 14: Ni ipi hukumu ya mtu anayemuomba asiyekuwa Allaah huku akiishi miongoni mwa waislamu na kwa lugha ya Qur-aan? Je, huyu ni muislamu aliyeingia kwenye shirki au ni mshirikina?

Jibu: Mtu huyu ni mshirikina, kwa sababu hana udhuru ikiwa anaishi miongoni mwa waislamu. Allaah (´Azza wa Jall):

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[1]

Kwa hiyo yule ambaye amfikiwa na Qur-aan basi hoja imemsimamia. Amesema (´Azza wa Jall):

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.”[2]

Yule ambaye amfikiwa na Qur-aan, amefikiwa na ulinganizi na akafanya shirki ilihali anaishi kati ya waislamu ni mshirikina.

Wanazuoni wengine wamesema kuwa mtu ambaye hajui kuwa ameingia kwenye shirki kwa sababu ya walinganizi wa upotovu na ushirikina na kwa sababu ya wingi wa wapotoshaji waliomzunguka na jambo hilo likawa limefichika kwake, basi katika hali hii jambo lake anaachiwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa msemo mwingine hukumu yake Ahl-ul-Fatrah ikiwa hakuwa na ujuzi. Hata hivyo ikiwa atafariki, atataamiliwa kama mshirikina. Kwa maana nyingine hatooshwa, hatoswaliwa na wala hatozikwa katika makaburi ya waislamu.

Kwa kifupi ni kuwa msingi ni kwamba hapewi udhuru. Lakini ikiwa kuna baadhi ya watu waliokuwa hawajui kwa sababu ya walinganizi wa shirki na upotovu na hawakujua, basi huenda ikasemwa kuwa mtu huyo ana udhuru katika hali hiyo na jambo lake anaachiwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hali yoyote ni wajibu kwake kutafuta haki, kujifunza haki na kuifuatilia kwa bidii kama anavyofanya bidii katika kujitafutia riziki na kuulizia njia za kujipatia kipato. Vilevile ni wajibu kwake kuuliza kuhusu dini yake na kuulizia jambo ambalo linamtatiza. Kusema kwamba hakusikia haki, hakukubali haki na alijifanya kiziwi dhidi ya kusikia haki, basi hili si udhuru kwake. Huu ndio msingi.

[1] 06:19

[2] 17:15

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 06/01/2026