14. Kwa nini Biblia ni maneno ya Allaah na si Qur-aan?

Nilikuwa mwanafunzi na mwenye kutoa hotuba katika chuo kikuu cha Bonn. Alikuwepo mwanafunzi myahudi akiitwa Yakobi. Alikuwa nusu myahudi. Kila ambaye mzazi wake mmoja alikuwa ni myahudi na mwingine ni mjerumani alikuwa akiitwa Hitler. Waliokuwa ni nusu mayahudi walikuwa na uhuru ambao mayahudi hawakuwa nao kipindi cha mateso. Kwa mfano hukumu juu ya mayahudi, ikiwemo kutosoma katika masomo ya kijerumani, zilikuwa haziwagusi. Hata hivyo wakuu wengi wa shule walikuwa wakiwakatalia kusoma kwa sababu ya chuki na dharau. Wengine walikuwa wakilichukulia suala hilo wepesi na wakiwaacha wasome.

Mkuu wa kitengo cha mashariki ya chuo kikuu cha Bonn alikuwa ni mmoja katika wenye kuchukulia wepesi suala hilo. Haikuwa mimi niliyeanza kumjengea chuki mtu huyu. Nilikuwa nikimwacha ahudhurie masomo yangu ya kiarabu na ya kiislamu. Yeye ndiye alianza kunionesha chuki. Si kwa jengine ni kwa sababu tu nilikuwa mwarabu.

Makamu wa mkuu alikuwa ni profesa mkatoliki aitwaye Hvnenk. Alikuwa akinichukia mimi kwa sababu ya mambo yafuatayo:

1- Tulikuwa ni wenye kutofautiana juu ya klasi ya masomo. Mudiri aliyetangulia alinipatia haki katika jambo hilo, jambo ambalo halisahau.

2- Akiwa akifunza kiebrania. Lakini mwalimu wake alikuwa ni Yakobi. Yakobi alikuwa ni nusu myahudi ndio maana alikuwa akijua kiebrania bora zaidi.

3- Wakati wa utawala wa Nazis wakatoliki walikuwa upande wa mayahudi. Yakobi alihisi kuwa ataweza kuniudhi, na akafanya hivo kweli.

Siku moja tulikuwa tumesimama kwenye maktaba. Yakobi akaleta Qur-aan, akaiweka juu ya meza na kusema:

“Tazama! Haya ni maneno ya Allaah!”

Akaanza kucheka na kujaribu kuwachekesha wengine, lakini hakuna yeyote aliyecheka. Nikasimama na kwenda kuleta mkusanyiko wa Taurati na Injili kwa kijerumani. Kwa nyuma vilikuwa vimeandikwa “Biblia takatifu”. Kwenye Qur-aan ilikuwa imeandikwa “Qur-aan ya Muhammad”. Nikaiweka Biblia karibu na Qur-aan. Kisha nikamgeukia na kumwambia:

“Myahudi! Ikiwa hii (yaani Taurati na Injili) ni maneno ya Allaah, basi hii pia (yaani Qur-aan) ni maneno ya Allaah. Sisi sio watoto wala wajinga ambao hawakusoma. Tumesoma kwenye vyuo vikuu. Tunajifunza kutafiti na kuhakiki. Vitabu hivi viwili vimekuja na watu wawili. Hali kadhalika na kitabu hiki. Kwa nini vitabu viwili hivi viwe ni vyenye kutoka kwa Allaah kwa kukata kabisa na hiki kingine iwe ni uongo wenye kukata kabisa juu ya Allaah? Vitabu hivi vimetujia kwa sura moja. Unafikiria kama ambaye si muweza.”

Yakobi akasema:

“Najua unachotaka kusema. Mimi ni mkristo protestant, sio myahudi kwa hali yoyote. Kanuni inakuadhibu kwa tuhuma hii.”

Nikasema:

“Ikiwa wewe sio myahudi, basi mimi ni myahudi.”

Waliokuweko pale wakaanza kucheka. Hakuweza kunifanya nicheke. Badala yake yeye ndo akacheka. Allaah alimlipiza kisasi vikali yeye na Hvnenk. Alikuwa akiishi Cologne. Alikuwa nyumbani pindi bomu la kingereza lilipoanguka nyumbani kwake. Familia nzima ikafa. Alinionyesha chuki ikiwa ni pamoja vilevile na kwamba pindi alipokuwa mkuu wa kitengo changu aliikataa shahada yangu ya udaktari ambayo ilipendekeza mkuu wa kabla yake. Nilitumika nayo kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hvnenk alipokuwa mkuu wa pale akasema kuwa kuna mtafiti kwenye chuo kikuu cha kingereza Cambridge ambaye tayari kishaandika kuhusu maudhui hayo. Nikamwambia kuwa sijui lolote kuhusu kazi ya mwingereza huyo na kwamba sintoandika kwa lugha ya kijerumani. Maprofesa wote katika kitengo cha mashariki wakamkaripia kwa hilo. Wakati nilipokuwa katika hali hiyo nikapata mwaliko kutoka kwenye redio ya Ujerumani mjini Berlin kupitia mkurugenzi wa redio ya kijerumani Cologne. Wanataka kufungua redio ya kijerumani kiarabu. Nikahama kwenda Berlin kama mwanafunzi, mhadhiri na mrejelewa wa lugha wa redio. Nikamaliza masomo yangu kupitia kwa profesa Hartmann. Allaah akanisalimisha kutokamana na shari ya huyu Hvnenk na Yakobi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 35-37
  • Imechapishwa: 16/10/2016