14 – Kusoma Qur-aan Tukufu

Dada yangu wa Kiislamu, soma sana Qur-aan Tukufu! Tambua ya kwamba ukisoma herufi moja, basi unapata kwayo jema moja na jema moja linalipwa mara kumi mfano wake. Hivo ndivo imethibiti katika Hadiyth Swahiyh.

Tambua ya kwamba watu wa Qur-aan ndio watu wa Allaah na waja Wake maalum, kwamba bora ya watu ni wale wenye kujifuza Qur-aan na wakaifunza na ataambiwa mtu wa Qur-aan siku ya Qiyaamah:

”Soma na upande na usome kama ulivyokuwa unasoma ulimwenguni! Kwani hakika ngazi yako ni katika ile Aayah ya mwisho.”

Ameipokea an-Nasaa´iy na wengineo.

Fanya pupa pia kuhifadhi sehemu katika Suurah za Qur-aan Tukufu.

Jifanyie ratiba ya sehemu unayoisoma kila siku.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 20
  • Imechapishwa: 11/02/2026