Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ

“Wanapopanda merikebu [wakakumbwa na misukosuko] basi humwomba Allaah kwa kumtakasia Yeye dini. Lakini anapowaokoa [kwa kuwafikisha salama] nchikavu, tahamaki hao wanamshirikisha.” (29:65)

MAELEZO

Shaykh ametaja dalili kuonyesha kuwa washirikina waliokuja nyuma wana shirki kubwa na ya khatari zaidi kuliko washirikina wa kale, kwa sababu washirikina wa kale walikuwa wakimtakasia ´ibaadah Allaah katika kipindi cha shida na wakimshirikisha wakati wa raha. Amejengea hoja maneno Yake (Ta´ala):

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Wanapopanda merikebu [wakakumbwa na misukosuko] basi humwomba Allaah kwa kumtakasia Yeye dini.”

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 35