14. Hadiyth ”Jitofautisheni na… ”

Abu Daawuud (1/247) amesema: Qutaybah bin Sa´iyd ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah al-Fazaariy ametuhadithia, kutoka kwa Hilaal bin Maymuun ar-Ramliy, kutoka kwa Ya´laa bin Shaddaad bin Aws, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jitofautisheni na mayahudi, kwani hakika wao hawaswali kwenye viatu vyao wala soksi za ngozi.”[1]

Ameipokea (kwa mujibu wa “Mawaarid-udh-Dhwamaan”, uk. 107) ya Ibn Hibbaan kwa ziada inayosema “na manaswara”, al-Bayhaqiy (2/423) na al-Haakim (1/26), ambaye amesema:

”Cheni ya wapokezi ya Hadiyth hii ni Swahiyh na wala hakuipokea al-Bukhaariy wala Muslim.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

kwa mujibu wa “Faydhw-ul-Qadiyr” amesema Haafidhw al-´Iraaqy kwamba “cheni yake ya wapokezi ni nzuri”.

at-Twabaraaniy ameipokea katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” (7/348) kwa tamko linalosema:

”Swalini kwenye viatu vyenu na wala msijifananishe na mayahudi.”

[1] Abu Daawuud (652) na Ibn Hibbaan (3186). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (652).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 15
  • Imechapishwa: 03/06/2025