14. Fadhilah za Tasbiyh, Tahliyl na Takbiyr

73 – Abu Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapofikiwa na jioni husema:

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر

”Tumeingiliwa na jioni na umekuwa ufalme ni wa Allaah, himdi zote ni stahiki ya Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee, hana mshirika. Ni Wake ufalme, na ni Zake  himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza.  Mola wa wangu, nakuomba kheri ya usiku wa leo, na kheri ya baada yake, na najilinda Kwako kutokamana na shari ya usiku wa leo na shari ya baada yake. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na uvivu, na uzee mbaya. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi.”[1]

MAELEZO

Hadiyth hii inajulisha kuwa Dhikr hii imewekwa katika Shari´ah asubuhi na jioni. Anapofikiwa na jioni atasema:

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله

”Tumeingiliwa na jioni na umekuwa ufalme ni wa Allaah… ”

na anapopambaukiwa atasema:

أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله

”Tumepambaukiwa na umekuwa ufalme ni wa Allaah… ”

Maana yake ni kutambua kuwa ufalme wote ni wa Allaah, Yeye ndiye Mwendeshaji na kwamba Yeye ndiye anayeyasimamia mambo yote.

[1] Muslim (2723).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 26/10/2025