Miongoni mwa vitu vinavyoonyesha unyenyekevu, udhalilifu na kujivunjavunja katika swalah ni kuweka mkono mmoja juu ya mwingine wakati wa kusimama. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu makusudio ya kufanya hivo akasema:

“Ni kujidhalilisha mbele ya Mshindi.”

´Aliy bin Muhammad al-Miswriy al-Waa’idhw (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sijawahi kusikia chochote kuhusu elimu kama hiki.”[1]

Imepokelewa Bishr al-Haafiy (Rahimahu Allaah) kwamba amesema:

“Kwa miaka arobaini nimetaka kuweka mkono mmoja juu ya mwingine ndani ya swalah yangu. Hakuna kinachonizuia kufanya hivo isipokuwa naona kuwa naonyesha unyenyekevu usiyokuwa ndani ya moyo wangu.”[2]

Muhammad bin Naswr al-Marwaziy (Rahimahu Allaah) amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

“Siku ya Qiyaamah watu watafufuliwa kwa mujibu wa matendo yao wakati wa kuswali.”[3]

Kwa maana ya kushika mkono wa kulia mkono wa kushoto na kuinama, hivo ndivo walivyofasiri baadhi ya wapokezi.

Vilevile amesimulia kwamba Abu Swaalih as-Samaan (Rahimahu Allaah) amesema:

“Watu siku ya Qiyaamah watafufuliwa namna hii.” Akaweka mkono mmoja juu ya mkono mwingine[4].

[1] Twabaqaat-ul-Hanaabilah (1/84).

[2] Taariykh Baghdaad (14/399).

[3] Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah (331).

[4] Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah (332).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 65-67
  • Imechapishwa: 24/11/2025