134. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na tatu wa al-An´aam

al-Qummiy amesema:

“Amesema:

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ

“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundimakundi, huna lolote kuhusiana na wao. Hakika amri yao iko kwa Allaah; halafu atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.”[1]

Walifarikiana na kiongozi wa waumini na wakawa mapote. Mama yangu amenihadithia, kutoka kwa Nadhwr bin Suwayd, kutoka kwa Yahyaa al-Halabiy, kutoka kwa Mu´liy bin Khunays, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

“Ninaapa kwa Allaah kwamba watu hawa wameifarikisha dini yao.”[2]

Ndio ni kweli. Shiy´ah wameifarikisha dini na wakawa mapote. Wamemtenga hata ´Aliy na wengine. Wale waliochupa mipaka katika wao kama vile Baatwiniyyah wameitenga dini yote na badala yake wakaipiga vita na wakawapiga vita wafuasi wao.

[1] 06:159

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/222).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 192
  • Imechapishwa: 14/07/2018