133. Wakati Jahm aliposoma Qur-aan

170 – Abu Nu´aym al-Balkhiy, simjui[1].

Yahyaa bin Ayyuub amesema: Abu Nu´aym al-Balkhiy, ambaye alikutana na Jahm, ametuhadithia:

”Jahm alikuwa na rafiki ambaye anamtukuza na kumtanguliza mbele ya wengine, ambapo bwana huyu akaanza kumsema vibaya na kumkejeli. Nikasema: ”Alikuwa akikutukuza.” Akasema: ”Kumetoka kwake mambo yasiyostahamiliwa. Wakati alipokuwa chumbani kwake akisoma Suurah Twaa Haa, akafika katika Aayah isemayo:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

Akasema: ”Lau ningepata njia ya kuifuta kutoka ndani ya msahafu basi ningefanya hivo.” Nikavumilia jambo hilo. Kisha wakati aliposoma Aayah nyingine akasema: ”Hakuwa mwema kwa Muhammad wakati Aliposema.” Halafu wakati aliposoma Suurah al-Qaswasw na msahafu ukiwa mapajani mwake, ikafikia kutajwa Muusa (´alayhis-Salaam), ambapo akausukuma msahafu kwa mkono wake na kuupiga teke na kusema: ”Mambo gani haya? Ametaja kisa cha Muusa sehemu mbili na hakukikamilisha!”

Kisha nikapata kuwa huyu Abu Nu´aym alikuwa ni Shujaa´ bin Abiy Naswr al-Muqri’, ambaye ni mmoja katika maswahiba wakubwa wa Abu ´Amr bin al-´Alaa’[3]. Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad as-Swaghaaniy, kutoka kwa Yahyaa bin Ayyuub[4].

32 – Abu Mu´aadh al-Balkhiy[5], mwanachuoni katika Fiqh.

171 – Ibn Abiy Haatim amesema: Zakariyyaa bin Daawuud bin Bakr ametuhadithia: Nimemsikia Abu Qudaamah as-Sarkhasiy akisema: Nimemsikia Abu Mu´aadh Khaalid bin Sulaymaan akisema Farghaanah:

”Jahm alikuwa kwenye njia panda za Tirmidh. Alikuwa anatokea Kuufah. Hakuwa na elimu yoyote wala mazowea ya kukaa na wanazuoni. Siku moja akakaa na wasameni, ambao wakamwambia: ”Tueleze kuhusu Mola wako unayemwabudu.” Akaingia nyumbani kwake na hakutoka isipokuwa baada ya masiku kadhaa.” Kisha akasema: ”Ni upepo huu, pamoja na kila kitu na ndani ya kila kitu. Hakosekani katika chochote.” Amesema uwongo adui wa Allaah. Bali Allaah yuko juu ya ´Arshi, kama alivyojielezea Mwenyewe.”[6]

[1] Bali anatambulika, kama ambavo mtunzi mwenyewe atayaashiria hayo.

[2] 20:05

[3] Alikuwa ni mkweli na mwaminifu kwa mujibu wa Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam. Ibn Hibbaan amemtaja katika “ath-Thiqaat”. Inavyonidhihirikia ni kwamba sio yule Abu Mu´aadh al-Balkhiy aliyetajwa katika “Lisaan-ul-Miyzaan”, ambapo imekuja:

“Mahmuud bin Ghaylaan amesema kuwa Ahmad, Ibn Ma´iyn na Abu Khaythamah wamezipiga chini Hadiyth zake na wakamwangusha.”

[4] Kupitia kwa Ibn Abiy Haatim, ambaye amesema: ´Abdullaah bin Muhammad bin al-Fadhwl al-Asdiy ametuhadithia: Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia Cheni hii ya wapokezi ni Swahiyh. al-Bukhaariy ameipokea katika “Khalqu Af´aal-il-´Ibaad”, uk. 71: Abu Ja´far (Muhammad bin ´Abdillaah) amenihadithia: Yahyaa bin Ayyuub amenihadithia. Cheni hii ya wapokezi pia ni Swahiyh na wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh. Abu Ja´far ni Muhammad bin ´Abdillaah bin al-Mubaarak al-Makhramiy. ´Abdullaah pia ameipokea katika ”as-Sunnah”, uk. 30, na cheni yake ya wapokezi pia ni Swahiyh pia.

[5] Miongoni mwa waalimu wake ilikuwa ni pamoja na ath-Thawriy na Ibn Jurayj. Mtunzi amesema katika ”Miyzaan-ul-I´tidaal”:

”Amedhoofishwa na Ibn Ma´iyn na wengine.”

[6] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Abu Qudaamah as-Sarkhasiy alikuwa ni mwenye kuaminika na mwenye kuhifadhi. Jina lake ni ´Abdullaah bin Sa´iyd al-Yashkuriy as-Sarkhasiy. Zakariyyaa bin Daawuud bin Bakr pia alikuwa madhubuti na ametajwa katika “al-Jarh wat-Ta´diyl” (1/2/602). Amefanyajiwa ufuatiliaji na Ibn Khuzaymah, kama alivyopokea al-Bayhaqiy katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 427-428.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 22/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy