Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Isitoshe mtu anatakiwa kutambua kuwa wale wapindishaji maana wanaoenda kinyume na Qur-aan, Sunnah na Salaf wako katika jambo la mkorogeko.
MAELEZO
Wanaopingana na Ahl-us-Sunnah katika mada ya majina na sifa za Allaah hawaafikiani kamwe. Kwa sababu wamefuata matamanio na akili zao. Matamanio pamoja na akili hutofautiana. Kila mmoja ana maoni yake, kila mmoja ana akili kwa kiwango chake inayopingana na akili ya mwingine na matamanio ya mwingine. Ndiyo maana wakatofautiana katika mada hii. Ama wale waliofuata Qur-aan na Sunnah hawatofautiani, kwa sababu hawakufuata matamanio na akili zao, bali wamefuata yaliyotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah. Ndio maana wakawa na umoja katika mada hii na nyenginezo. Hii ndiyo siri ya kuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawakutofautiana katika mada ya a majina na sifa za Allaah, na kwamba makundi mengine yametofautiana. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ
“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake!”[1]
Akaifanya njia Yake kuwa moja isiyotofautiana. Wala hawatofautiani wanaoifuata. Akafanya njia zingine zote kuwa nyingi zisizo na hesabu. Aidha Akaeleza kwamba zinawatenganisha watu wake. Hivyo hutakuta kundi moja linaafikiana na kundi jingine. Mwisho wake makundi yote hayafikii matokeo yoyote. Ndiyo maana Allaah amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):
بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَّرِيجٍ
”Bali wamekadhibisha haki pale ilipowajia, basi wao wamo katika jambo la mkorogeko.”[2]
Kwa maana lenye tofauti, lenye kupingana na lenye mgongano. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ
”Watakapoamini kama vile mlivyoamini nyinyi, basi kwa hakika watakuwa wameongoka. Na wakikengeuka, basi hakika wao wamo katika upinzani.”[3]
[1] 6:153
[2] 50:05
[3] 2:137
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 221
- Imechapishwa: 14/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 221
Imechapishwa: 14/07/2026
https://firqatunnajia.com/133-ndio-maana-ahl-us-sunnah-wakawa-wamoja-na-ahl-ul-bidah-wakatofautiana/